[ad_1]
TUSIJE TUKASAHAU: Serikali ikomeshe hii hadaa ya vipakatalishi
NA CHARLES WASONGA
MNAMO Jumatano wiki hii Katibu katika Wizara ya Elimu anayesimamia Elimu ya Juu Simon Nabukwesi alitangaza kuwa serikali itaanzisha mpango wa usambazaji wa vipakatalishi kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vyote vya umma nchini.
Akihutubu katika Shule ya Upili ya Sipala eneobunge la Webuye, kaunti ya Bungoma, Bw Nabukwesi alisema kuwa wanafunzi hao hawatatozwa ada zozote kwa vifaa hivyo.
Lakini afisa huyo asije akasahau kuwa mpango sawa na huo ambao serikali hii hii ya Jubilee iliahidi kuanzisha katika shule za msingi kuanzia 2013 haukufaulu kwani ulizongwa na ufisadi. Hii ni licha ya mpango huo kufyonza mabilioni ya fedha.
Wakati wa kampeni za kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huo, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliahidi kuwa wanafunzi wa darasa la kwanza watapewa vipakatalishi hivyo kufanikilisha masomo ya kidijitali.
Bw Nabukwesi anapotoa ahadi sawa na hiyo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza, Waziri wa Fedha Ukur Yatani juzi ametangaza kuwa serikali itapunguza ufadhili kwa vyuo vikuu vya umma.
Next article
Wazee kumbariki Ruto huku Gideon akibaki na rungu
[ad_2]
Source link