Connect with us

General News

Serikali isilegeze kamba inapokabili wahuni katika bodaboda – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Serikali isilegeze kamba inapokabili wahuni katika bodaboda – Taifa Leo

TAHARIRI: Serikali isilegeze kamba inapokabili wahuni katika bodaboda

NA MHARIRI

MSAKO wa polisi unaoendelea nchini dhidi ya wahudumu wa bodaboda unapasa kudumishwa hadi wahalifu wote ambao wamegeuza sekta hiyo ndogo, lakini muhimu, kuwa maficho yao wafurushwe.

Ni kweli kwamba, wahudumu wa bodaboda hutekeleza wajibu muhimu katika uchukuzi wa umma. Wamerahisisha usafiri hasa katika maeneo ambapo hamna magari ya uchukuzi. Wahudumu hao vile vile, mara nyingi hutumika kama tarishi na wateja ambao wanahitaji huduma fulani kwa dharura.

Hata hivyo, kuna maelfu ya wengine ambao wamepaka tope sekta hiyo. Kwa kuwa hamna sheria mahususi za kuisimamia, wahalifu wengi hutafuta maficho yao huko. Tukio la hivi majuzi ambapo mwanamke mwendeshaji gari alivamiwa na kuvuliwa nguo na watu waliojifanya kuwa wanabodaboda ni ithibati tosha kwamba, kuna wahalifu wengi mno wanaojisawiri kama waendeshaji pikipiki.

Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Kitaifa cha Utafiti Kuhusu Jinai, (NCRC) bodaboda wengi husababisha vifo kwa kuendesha pikipiki bila uangalifu, asilimia 79 hushiriki katika visa vya wizi, asilimia 66 huzua vurugu na kutatiza amani, asilimia 66 hujihusisha katika visa vya wizi wa mabavu huku asilimia 49 wakiuza na kutumia mihadarati hatari.

Visa vingine vya uhalifu ambavyo waendesha pikipiki hao wamehusishwa navyo ni utekaji nyara, unajisi na ulanguzi wa bidhaa kwenye sehemu za mpakani huku asilimia 12 wakiripotiwa kupokea mali ya wizi.

Tunapongeza hatua ya Waziri wa Usalama wa Ndani, Dkt Fred Matiang’i kuanzisha upya mchakato wa kusajili wahudumu hao kote nchini. Hii ni hatua nzuri ambayo itaondoa wahalifu ambao wamejisitiri miongoni mwa bodaboda hao.

Ni matumaini yetu kwamba, mapendekezo ya jopokazi lililoteuliwa kumulika sekta hii pia yatachunguzwa na ikiwa yataonekana kufaa, basi yatekelezwe.

Wakati wa kusafisha uozo uliosakama sekta hii ni sasa na wanaopanga kuhujumu mchakato huo wanapasa kuadhibiwa vikali kwa mujibu wa sheria za nchi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending