[ad_1]
TUSIJE TUKASAHAU: Serikali yafaa kufuata sheria za kudhibiti biashara ya vyuma kuu kuu
NA CHARLES WASONGA
JUZI, Rais Uhuru Kenyatta alipiga marufuku biashara ya vyuma vikuukuu nchini ili kumaliza visa vya uharibifu wa miundo msingi muhimu kama nguzo za kusambaza umeme na kusababisha kupotea kwa umeme.
Rais alisema hatua hiyo itaendelea kutekelezwa hadi wakati serikali itaweka mwongozo utakaohakikisha kuwa vyuma vinavyouzwa sio vile vinavyoibiwa kutoka kwa nguzo za stima, reli au barabara.
Lakini Rais Kenyatta asije akasahau kwamba kuna Sheria ya Kudhibiti Biashara ya Vyuma Vikuu Kuu (Scrap Metal Act) ambayo yeye mwenye aliitia saini mnamo Novemba 13, 2013.
Sheria hiyo inapendekeza kubuniwa Baraza la Kusimamia Biashara ya Vyuma Vikuu Kuu, kusimamia masuala yote katika sekta hiyo ndogo.
Kabla ya hapo bunge la 11 lilipitisha Sheria ya Kawi na Mawasiliano ya 2011 kuzuia uharibifu wa nyaya za umeme na mawasiliano.
Kwa hivyo, serikali inapaswa kutekeleza sheria hizi kikamilifu badala ya kuweka marufuku inayoathiri hata wale wanaotii sheria zilizoko sasa.
Next article
Bodi ya KPLC yapigwa darubini kuhusu kupotea kwa umeme
[ad_2]
Source link