Connect with us

General News

Serikali yaondoa marufuku dhidi ya biashara ya vyuma chakavu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Serikali yaondoa marufuku dhidi ya biashara ya vyuma chakavu – Taifa Leo

Serikali yaondoa marufuku dhidi ya biashara ya vyuma chakavu

NA CHARLES WASONGA

SERIKALI imeondoa marufuku iliyoweka dhidi ya biashara ya vyuma chakavu mnamo Januari 20, 2022.

Hata hivyo, wafanyabiashara wote wa vyuma hivyo sharti wakaguliwe katika ngazi ya kaunti kabla ya kuruhusiwa kuanza kazi kuanzia Mei 1, 2022.

Waziri wa Ustawi wa Kiviwanda Betty Maina alitangaza kuondolewa kwa marufuku hayo yaliyowekwa na Rais Uhuru Kenyatta kufuatia kisa ambapo vyuma vya nguzo ya nyaya za stima viliharibiwa na kuibiwa na wahalifu, hali iliyosababisha kupotea kwa stima kote nchini.

Jumla ya wahandisi 12 wa kampuni ya Kenya Power walikamatwa kuhusiana na uovu huo ambao ulitokea katika eneo la Embakasi, Nairobi.

Bi Maina alisema kuwa mtu yeyote ambaye atapatikana akishiriki biashara ya kununua na kuuza vyuma chakavu bila kibali ataadhiwa kwa kutozwa faini isiyozidi Sh20 milioni.

“Mtu yeyote ambaye ataendesha biashara hii bila leseni atakuwa anafanya kosa na atatozwa faini ya hadi ya Sh20 milioni kama hatua ya kuhakikisha kanuni zilizowekwa zinazingatiwa,” akasema Bi Maina, kwenye kikao na wanahabari afisini mwake Nairobi.

Waziri Maina alisema kuwa wafanyabiashara wote waliotuma maombi ya leseni watapigwa msasa na makundi ya maafisa kutoka idara mbalimbali katika ngazi ya kaunti. Maafisa hao wataongozwa na makamishna wa kaunti katika kila kaunti.

Marufuku hiyo inaondolewa mwezi mmoja baada ya waziri wa usalama Fred Matiang’I kutangaza kwa wafanyabiashara wa vyuma vikuu kuu sharti wapewe leseni mpya.

Alisema ni baada ya wafanyakazi hao kufanyiwa ukaguzi na kupewa leseni mpya ambapo wataruhusiwa kufungua biashara zao.

Mnamo Aprili 5, wafanyabiashara wa vyuma vikuu kuu walifanya maandamano jijini Nairobi walishinikiza Rais Uhuru Kenyatta aondoe marufuku hiyo ili kuwakinga na hasara zaidi.

Wakiongozwa na alikuwa Mbunge wa Embakasi Kusini Irshad Sumra, wafanyakazi hao ambao ni wanachama wa Muungano wa Wafanyabiashara wa Vyuma Vikuu Kuu Nchini (KISMA), walidai kuwa wamepata hasara ya zaidi ya Sh800 milioni tangu marufuku hiyo kuwekwa mnamo Januari 20, 2022.

“Tunataka Rais Kenyatta atusaidie sisi ambao tuko na leseni ili turejee kazini. Baadhi yetu tulikopa pesa ili tupate leseni hizo. Tunaomba Rais atupe angalau siku 60 ili tuuze vyuma ambavyo tulikuwa navyo kwenye stoo zetu,” akasema Bw Sumra.