Connect with us

General News

Serikali yasisitiza kunayo chanjo ya mifugo kwa wingi, yaonya walaghai – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Serikali yasisitiza kunayo chanjo ya mifugo kwa wingi, yaonya walaghai – Taifa Leo

TAARIFA ZA WIKI: Serikali yasisitiza kunayo chanjo ya mifugo kwa wingi, yaonya walaghai

NA LEONARD ONYANGO

SERIKALI imewahakikishia wakulima kuwa kuna chanjo ya mifugo ya kutosha nchini.

Kulingana na Dkt Geoffrey Kamau, mwenyekiti wa bodi ya Taasisi ya Uzalishaji Chanjo ya Mifugo Nchini (Kevevapi), chanjo ya mifugo na ndege inayozalishwa humu nchini ina ubora wa juu.

Dkt Kamau alisema kuwa taasisi hiyo imetengeneza chanjo zinazokubalika hata katika masoko ya kimataifa.

Chanjo hizo zinakabiliana na maradhi kama vile homa ya matumbo kwa kanga, ‘Gumboro’ kwa vifaranga wa kuku na batamzinga na ugonjwa wa miguu na mdomo kwa ng’ombe.

Alisema kuwa taasisi hiyo inashirikiana na serikali kupambana na madaktari feki wa mifugo ambao wamekuwa wakiwasababishia wakulima hasara kwa kutoa chanjo bandia kwa mifugo wao.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending