Connect with us

General News

Sheikh akataa kutoka Kamiti – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Sheikh akataa kutoka Kamiti – Taifa Leo

Sheikh akataa kutoka Kamiti

NA RICHARD MUNGUTI

MWALIMU wa dini ya Kiislam kaunti ya Marsabit aliyekamatwa 2018 na kushtakiwa kwa ugaidi Alhamisi aliishangaza mahakama alipokataa kutoka gereza kuu la Kamiti baada ya kuachiliwa huru huku akidai atauawa na maafisa wa polisi.

Kufuatia kukataa kwake hakimu mkuu mahakama ya Nairobi Bi Wendy Kagendo aliamuru Sheikh Guyo Garso aendelee kuzuiliwa katika gereza hilo kwa muda wa siku 30 hadi mahakama kuu itakapoamua kesi aliyoshtaki akiomba alindwe na Serikali asiuawe.

Sheikh Garso alieleza hakimu anahofia maisha yake na “angependelea kuishi katika gereza la Kamiti asiuawe vile washukiwa wengine wa ugaidi walivyouawa.”

Bi Kagendo alikubalia ombi la Mwalimu huyo wa Madrassa aliyeshikwa na kushtakiwa kwa kutoa mafunzo yenye itikadi kali.

Hakimu alimwagiza mshtakiwa ajigharimie chakula na mahitaji mengine anapoendelea kukaa katika Gereza la Kamiti.

“Kwa vile hii mahakama imekuachilia, hauko mikononi mwa maafisa wa idara ya magereza. Sasa itabidi ujigharimie mahitaji yako kitambo mahakama kuu iamue hatima yako,” Bi Kagendo aliagiza.

“Nataka uelewe kwamba hii mahakama imekuachilia. Uko huru sasa. Unaweza ukaenda nyumbani ama urudi Kamiti vile utakavyochagua. Ikiwa utalipa idara ya magereza pesa za kugharimia mahitaji yako nitaweka sahihi stakabadhi uendelee kukaa Kamiti,” alisema Bi Kagendo.

Akimruhusu Sheikh Garso kuendelea kukaa gerezani, Bi Kagendo alisema “haifai kumwachilia mwalimu huyo wa dini huru ilhali anadai yuko na habari za kuaminika kwamba akiachiliwa huru atauawa.”

Wakili Dkt John Khaminwa aliyemwakilisha Sheikh Garso katika kesi hiyo alimweleza hakimu “huyu mwalimu wa madrasa anahofia maisha yake.”

“Amenieleza yuko na hakika ukimwacha huru atatoweka kama vile washukiwa wengine wa ugaidi walivyotoweka na hawajulikani waliko. Wameuawa kwa vile tangu watiwe nguvuni na maafisa wa polisi wa kupambana na ugaidi (ATPU) hawajawahi rudi nyumbani na hawasikiki kamwe,” akasema Dkt Khaminwa.

Wakili pia alimweleza hakimu mahakama iko na jukumu la kulinda maisha ya wananchi.

Sheikh Garso mwenye umri wa miaka 56 aliachiliwa katika mashtaka 11 ya kupatikana na kaseti 28 zenye mafunzo ya itikadi kali ya ugaidi.

Akinukuu vifungu 20, 21 na 22 vya Katiba Dkt Khaminwa alisema asasi za serikali ziko na wajibu wa kulinda haki za wananchi.

Dkt Khaminwa alimweleza hakimu kwamba atalipa idara ya magereza ili Sheikh Garso aendelee kuzuiliwa katika gereza hilo.

Mhubiri huyo alionekana mwenye wasi wasi hata alipokuwa anatoka kizimbani.

Watu wa familia yake walieleza hofu akiachiliwa atatoweka.

“Tunaomba aendelee kukaa Kamiti mahala tutakapokuwa tunamtembelea na kumwona akiwa hai,” mmoja wa watu wa familia yake alieleza.

Dkt Khaminwa alisema amewasilisha kesi katika mahakama kuu akiomba agizo mshtakiwa atunzwe na Serikali.

Wiki mbili zilizopita Dkt Khaminwa alikuwa ameomba Bi Kagendo amwachilie mshtakiwa kisha aandamane naye ampe makao nyumbani kwake Karen.

Kesi hiyo itatajwa Juni 6, 2022 ibainike ikiwa mahakama kuu imetoa maagizo atakakoishi Sheikh Garso.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending