Connect with us

General News

Sheng inafaa kupigwa marufuku miongoni mwa wanafunzi nchini? – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Sheng inafaa kupigwa marufuku miongoni mwa wanafunzi nchini? – Taifa Leo

NGUVU ZA HOJA: Sheng inafaa kupigwa marufuku miongoni mwa wanafunzi nchini?

NA PROF IRIBE MWANGI

JANA – Jumatano – nilikutana na wawili wa wanafunzi wangu wa zamani.

Tulianza kuzungumzia mustakabali wa sasa wa Kiswahili katika taasisi za elimu. Walikubaliana kwamba Kiswahili Sanifu kinaborongwa sana.

Baada ya mazungumzo marefu, walikubaliana pia kwamba kuna umuhimu wa kupigwa marufuku matumizi ya Sheng miongoni mwa vijana.

Baada ya maafikiano hayo mmoja wao aliniuliza, “Lakini Profesa, Sheng kweli ni lugha?”

Hili ni swali muhimu ambalo nililipambanua kwa kirefu na kwa kutumia mikabala tofauti tofauti, hata hivyo, hapa naomba nitaje tu kwamba kusudi kubwa kabisa la lugha ni mawasiliano baina ya wahusika.

Kwa sababu hiyo, swali la kujiuliza ni je, watumizi wa Sheng huwasiliana?

Baada ya kulijibu swali lao, nami niliuliza langu, je pendekezo hilo lao la kupigwa marufuku Sheng miongoni mwa vijana litatekelezwa vipi?

Na nani? Tulikubaliana kwamba utekelezaji wa kanuni kama hiyo ni jambo lisilowezekana. Nilipiga hatua na kueleza kwamba si tu kwamba haliwezi bali halitekelezeki, lakini pia si muhimu.

Daima lugha mbalimbali zimekuwepo na kila lugha huwa na majukumu yake. Mbali na majukumu, kila lugha huwa na uwanja au muktdha wa matumizi. Sheng basi ina majukumu yake, watumizi wake na muktadha wake wa matumizi.

Badala ya kujaribu kutatiza matumizi yake, inafaa ieleweke katika mazingira yake na kukubalika. Si lazima kila mtu aielewe. Kwa hakika hatuelewi lugha zote lakini hicho si kikwazo dhidi ya mawasiliano. Muhimu ni kutoa nafasi ya matumizi ya Sheng na kuitofautisha na Kiswahili sanifu. Kila mojawapo ina nafasi na mahali pake.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending