Connect with us

General News

Shirika latoa wito Wakenya wafuatilie kampeni za uchaguzi bila vurugu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Shirika latoa wito Wakenya wafuatilie kampeni za uchaguzi bila vurugu – Taifa Leo

Shirika latoa wito Wakenya wafuatilie kampeni za uchaguzi bila vurugu

NA LAWRENCE ONGARO

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Kenya Alliance of Resident Association (KARA), limetoa wito kwa Wakenya likiwataka wawe waangalifu wasije wakachochewa na viongozi wachache.

Kanali mstaafu wa jeshi Bw Julius Gathiri alieleza kuwa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022 mambo mengi yanashuhudiwa na kwa hivyo kila mmoja ana jukumu la kuwa macho.

“Ninatoa ushauri kwa vijana ambao ndio hulengwa kuzua vurugu wawe chonjo wasije wakatumiwa vibaya na viongozi hao wanaojitakia makuu. Wasikubali kupewa vileo ama dawa za kulevya ili walete vurugu wakati wa uchaguzi,” alisema Bw Gathiri.

Aliyasema hayo Ijumaa, shirika la KARA lilipofanya kongamano huku washika dau na wakazi wa Thika wapatao 100 wakihudhuria.

Aliwashauri wananchi popote walipo waelewe haki zao ili wasije wakapotoshwa na viongozi wanaotafuta vyeo vya uongozi kwa kutumia kila njia.

Shirika latoa wito Wakenya wafuatilie kampeni za uchaguzi bila vurugu. PICHA | LAWRENCE ONGARO

Alisema matukio ya vurugu hushuhudiwa katika mitaa ya mabanda na kwingineko ambako vijana hawana ajira.

“Pengo kubwa kati ya matajiri na maskini pia linachangia pakubwa vijana wengi kutumiwa vibaya na viongozi ili kushiriki machafuko. Kwa hivyo kuna haja ya vijana kupewa hamasisho ili waelewe ukweli wa mambo,” alifafanua Bw Gathiri.

Mtaalam wa maswala ya mawasiliano na habari Bw Frederick Okango, aliwashauri wananchi wawe mstari wa mbele kuwadadisi viongozi na kuwauliza maswali ili kungundua ni lipi wanalotaka kutendea Wakenya.

Alitoa mwito kwa waandishi wa habari kuandika mambo yaliyo na ukweli badala ya kutumia uvumi ya mambo waliyosikia.

Aliwashauri wananchi watathmini kwa makini maneno yanayonenwa na viongozi, ili wasije wakapotoshwa.

Waandishi wa habari pia walihimizwa wasije wakaandika habari za uchochezi zinazoweza kuleta uhasama miongoni mwa makabila tofauti nchini.

Afisa mkuu wa Shirika la (KARA) Bw Henry Ochieng’, alisema afisi yake imejitolea kuzunguka nchini ili kuhamasisha Wakenya kuhusu haki zao bila kupotoshwa.

Alisema kwa sasa wanalenga vijana ambao ndio hutumiwa vibaya inapofika wakati wa uchaguzi.

Alieleza kuwa wamejitokeza kushirikiana na washika dau wote hapa nchini ili kuhakikisha ujumbe wao unafikia wananchi walioko mashinani.

Mwanaharakati wa kupambana na walioathirika na ulevi na dawa za kulevya, Bi Gladys Chania, aliwahimiza vijana wawe makini wasije wakapotoshwa kwa kupewa pombe ili wazue machafuko.

“Ninawahimiza vijana wasije wakapotoshwa na viongozi wanaojitakia makuu bila kujali maslahi ya wananchi,” alifafanua Bi Chania.

Mwanasaikolojia huyo anayewania kiti cha Mwakilishi wa Kike katika kaunti ya Kiambu, anasema atafanya juhudi kukutana na vijana mashinani ili kuwahamasisha kuhusu haki zao.

Aliwashauri wanawake wanaotaka uongozi wajitokeze wazi bila kuogopa lolote.

“Huu ndio wakati wa wanawake kujitokeza na kutafuta uongozi. Kwa hivyo ni vyema kujitokeza wazi bila uwoga wowote,” alieleza Bi Chania.

Alitaka serikali kuwapa wanawake ulinzi hasa wakati huu kuelekea uchaguzi wa Agosti 9, 2022.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending