Eneo la kibiashara la Turi. Wakazi wanahofu baada ya visa 18 vya Covid-19 katika shule jirani ya St Andrew’s Turi. Picha: Maryyanne Ndunge Source: Facebook
Mbunge wa Molo Kuria Kimani aliwataka wakazi kuwa watulivu akiwahakikishia kuwa suala hilo linashughulikiwa na sekta ya afya.
“Watu hao ni wafanyakazi wa St Andrew’s Turi. Wizara ya Afya inafanya kila iwezalo kuwatafuta waliotengamana na wagonjwa hao ili kuepuka kusambaa kwa ugonjwa huo,” alisema Kimani.
Mbunge huyo aliongeza kuwa waliopatikana na virusi hivyo ni wafanyakazi ambao huishi shuleni humo.
Shule hiyo ni mojawapo wa shule za kifahari humu nchini. Source: UGC
Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa eneo hilo ni wafanyakazi pia kwenye shule hiyo na kuna wasiwasi wa iwapo walitengamana na wagonjwa na kisha kurudi kwa familia zao.
Mfanyibishara wa Turi Salaons Lempaa alisema shule hiyo inafaa kutengwa mara moja ili kuepuka maambukizi.
“St Andrew’s Turi inafaa kutengwa mara moja kuzuia wafanyakazi kurudi nyumbani na kuendeleza maambukizi kwa familia zao,” alisema Lempaa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.