Gavana Mike Sonko na Rais Uhuru Kenyatta katika picha ya awali. Picha: Mike Sonko Source: Facebook
Sonko alisema kilichotokea nchini Burundi ambapo Rais Pierre Nkurunziza alifariki kutokana na covid-19 ni dhihirisho kuhusu hatari ya ugonjwa huo.
Alilaumu Nkurunziza akisema wakati mataifa mengine yalikuwa yakitafuta mbinu za kupigana na ugonjwa huo, nchi hiyo iliamua kushiriki mchakato wa kampeni za urais.
“Wakati Rais Uhuru Kenyatta na nchi zingine walikuwa wakitafuta njia za kukabili kusambaa kwa covid-19, Burundi ilikuwa inashiriki uchaguzi bila hata kuzingatia maagizo ya shirika la Afya duniani kuhusu kukabili janga hili,” Sonko alisema.
Msemaji wa Ikulu Kanze Dena alisema Rais na familia yake wako salama. Picha: State House Source: Twitter
Gavana huyo aliwataka wenzake ambao walihudhuria mkutano wa Ikulu pamoja na Rais Kenyatta kufanyiwa ukaguzi ili kujua hali yao.
“Nawaomba wenzangu ambao tulihudhuria mkutano Ikulu Juni 10 kujiweka karantini na kupimwa covid-19 kabla ya kutengamana na wafanyikazi wa kaunti,” alisema Sonko.
Msemaji wa Ikulu Kanze Dena alitangaza kuhusu wafanyikazi hao waliopatikana na coronavirus lakini akahakikishia Wakenya kuwa Rais na familia yake wako salama.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.