Connect with us

General News

Southampton wachapa Aston Villa ligini na kuweka kocha Smith katika hatari ya kufutwa kazi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Southampton wachapa Aston Villa ligini na kuweka kocha Smith katika hatari ya kufutwa kazi

Southampton wachapa Aston Villa ligini na kuweka kocha Smith katika hatari ya kufutwa kazi

Na MASHIRIKA

BAO la mapema kutoka kwa Adam Armstrong lilisaidia Southampton kuendeleza ufufuo wao katika kampeni za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kuwapokeza Aston Villa kichapo cha tano mfululizo ligini.

Chini ya kocha Dean Smith, Villa walianza kampeni zao vibaya huku masihara ya Matt Cash yakichangia bao lilifumwa wavuni na Armstrong katika dakika ya tatu.

Villa walikuwa hoi katika kipindi cha kwanza na Southampton wangalifunga mabao mengi zaidi baada ya Anwar el Ghazi na Emiliano Buendia kupoteza nafasi kadhaa za kuwaweka Villa kifua mbele.

Ushindi wa Southampton uliwapaisha hadi nafasi ya 12 huku Villa wakisalia na alama tatu pekee juu ya mduara unaojumuisha vikosi vitatu vya mwisho jedwalini.

Villa walikuwa wakijivunia alama sita zaidi kuliko Southampton mwanzoni mwa Oktoba 2021. Kwa sasa wana pointi 10, nne nyuma ya Southampton ya kocha Ralph Hasenhuttl ambaye ameongoza waajiri wake kuzoa alama 10 kutokana na mechi nne zilizopita ligini.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending