[ad_1]
Spurs na Southampton nguvu sawa katika gozi la EPL
Na MASHIRIKA
KOCHA Antonio Conte amesema Tottenham Hotspur “wanahitaji kujiimarisha zaidi” na “haitakuwa rahisi kwa kikosi chake kupigania taji lolote muhula huu” baada ya kulazimishiwa sare ya 1-1 na Southampton katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Jumanne.
Chini ya kocha Ralph Hasenhuttl, Southampton walitandaza mchuano huo kwa zaidi ya dakika 50 wakiwa na wachezaji 10 pekee uwanjani baada ya Mohammed Salisu kumchezea visivyo fowadi Son Heung-min na kuchangia penalti iliyofumwa wavuni na mvamizi Harry Kane.
Mechi hiyo ilimwezesha kocha Antonio Conte kuweka rekodi ya kuwa mkufunzi wa kwanza katika historia ya Spurs kutoshindwa katika mechi saba za kwanza ligini.
“Yasikitisha kwamba hatukushinda mechi licha ya kucheza vizuri. Sasa tuna ulazima wa kujinyanyua upesi katika mechi zijazo na kuweka hai matumaini ya kuwa miongoni mwa vikosi vinne vya kwanza kwenye msimamo wa jedwali la EPL mwishoni mwa msimu huu,” akasema kocha huyo wa zamani wa Chelsea, Juventus na Inter Milan.
Chini ya Conte, Spurs kwa sasa wameshinda mechi nne na kuambulia sare mara tatu kwenye kampeni za EPL. Kikosi hicho kinashikilia nafasi ya kwa alama 30, tano zaidi nyuma ya Arsenal wanaofunga mduara wa nne-bora. Hata hivyo, Spurs wana mechi mbili zaidi za kutandaza ili kufikia idadi ya michuano ambayo imesakatwa na Arsenal ambao ni watani wao wakuu kutoka London Kaskazini.
Southampton ambao wamepoteza mechi moja pekee katika uwanja wao wa nyumbani wa St Mary’s kufikia sasa msimu huu, wanakamata nafasi ya 13 kwa pointi 21. Kikosi hicho kiling’atwa na Wolves kwa bao 1-0 mnamo Septemba 26, 2021.
TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO
Next article
Vijana 200 wa Thika wakamilisha kozi za kuwafaa maishani
[ad_2]
Source link