Connect with us

General News

SS Assad halahala kuweka historia ya kutua ligini KPL – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

SS Assad halahala kuweka historia ya kutua ligini KPL – Taifa Leo

SS Assad halahala kuweka historia ya kutua ligini KPL

Na ABDULRAHMAN SHERIFF

KAMA kuna timu iliyowakosha sana wapenzi wa soka Pwani msimu jani, ni SS Assad FC ambayo iliongeza idadi ya klabu zinazoshiriki Ligi ya Kitaifa ya Supa (NSL).

Timu hiyo iliyoko mjini Ukunda, Kaunti ya Kwale, iliwashangaza mno mashabiki ambao hawakuwa na matumaini yoyote kwake kufana Ligi ya Kitaifa Daraja ya Kwanza, ikifanikiwa kumaliza nambari mbili.

Meneja Hamisi Dele aliambia Dimba kuwa, msimu uliopita walipania kuhakikisha kama si ushindi basi wafuzu kupanda ngazi hadi Supaligi (NSL), na wamefurahi mno kutimiza lengo lao.“Ninaamini kama tulivyotia bidii kupanda ngazi, tuna nia iyo hiyo ya kujitahidi kupanda ngazi hadi Ligi Kuu Nchini (KPL).

“Si hoja kwamba ni mara ya kwanza tunashiriki ligi hii ya NSL; tutafanya bidii ili tushinde au tumalize nafasi nzuri,” alisema Dele.Ili kuimarisha kikosi kwa kivumbi wanachotarajia NSL, Assad wamesajili wanasoka watano kutoka timu mbalimbali.

“Tumesajili wachezaji hao wapya sababu tunataka kukiimarisha kikosi kipate kuwika,” akaeleza meneja huyo.Wachezaji wao wapya ni pamoja na aliyekuwa golikipa wa Bandari FC, Omar Abdalla, Ali Juma Mwazizi kutoka Fortune Sacco FC, Shaaban Mwachozi aliyekuwa na Coast Stima (ambayo sasa inaitwa Coastal Heroes) na wawili ambao hawakuwa na klabu, Omar Marere na Juma Tsala.

Kikosi kizima cha timu hiyo kwa msimu huu katika NSL ni Abdalla Juma (Nahodha), Ali kesi, Shaib de Gea, Joakim Daily, Juma Mwajao, Abdalla Hindo, Suleiman Ahmed, Sunday Mwaila, Abdalla Hamad Mdeka na Zakaria Mwakisu.

Wengine ni Ali Juma, Salim Dele, Rama Salim, Salim Zaire, Mathias Matabu, Briton Kitemwa, Matano Nuh Tele, Sadik Mwachotea, Ali Mwazizi, Hemedi Mwatsingwa, Heri Said, Idd Said, John Ebong na Ridhwan Mohamed.

Kocha Ali Marumu asema ingawa hawakupata muda wa kutosha kujitayarisha msimu ulipotamatika, sababu ya kumaliza mechi za Ligi ya Daraja ya Kwanza kuchelewa, ana imani na kikosi chake.“Najua vijana wangu hawakupata muda wa kutosha wa kupumzika, lakini watafanya juhudi kutamba,” akasema Marumu.

Naye mkufunzi wa magolikipa Hatibu Chabindo – ambaye aliwahi kushikilia wadhifa kama huo kambini mwa Bandari FC, baada ya kustaafu kuwa kipa wa vigogo wa ligi kuu – anaeleza kuwa walinda-lango wake wako sawa na watahakikisha wanafana NSL.

“Nina imani kwaamba, kufuatia mafunzo niliyowapa wataonyesha ni nyani langoni, na hata wakifungwa yatakuwa mabao machache tu,” alihoji Chabindo.Maafisa wa soka Kwale pamoja na mashabiki wana hamu kubwa Assad FC ifanikiwe katika NSL, ili iweke historia ya kuwa timu ya kwanza ya kaunti hiyo kufuzu kushiriki ligi kuu KPL.

Katibu wa Shirikisho la Soka (FKF) Kaunti ya Kwale, Shilingi Fumbwe, pamoja na mwakilishi wa soka ya wanawake tawi hilo Fatma Mwinyi wana hamu kubwa Assad FC ifanikiwe kuweka historia, ya kuwa timu ya kwanza ya Kwale kufuzu kushiriki ligi kuu KPL.

Nalo Shirikisho la Soka la nchini (FKF) tawi la Kaunti ya Kwale limeahidi kushirikiana kikamilifu na maafisa wa Assad kuhakikisha klabu hiyo inapata udhamini ili isiwe na matatizo ya gharama za ushiriki katika ligi hiyo.

Mwenyekiti wa FKF Kwale, Hamisi Mwakoja amesema watajitahidi na kushirikiana na maafisa wa Assad katika harakati za kuitafutia klabu hiyo udhamini ili wachezaji wapate kucheza soka ya hali ya juu kupigania kupanda ngazi hadi Ligi Kuu ya Kenya.

“Ninaamini kwa ushirikiano wetu na wakuu wa klabu tunaweza kufanikiwa kuipatia timu yetu hiyo udhamini ambao utaisaidia isipate tatizo la kusafiri ama gharama nyingine muhimu kwa timu ya NSL kuwa nayo,” akasema Mwakoja.

Katibu wa tawi hilo, Shilingi Fumbwe pamoja na mwakilishi wa soka ya wanawake Fatma Mwinyi walisema wana hamu kubwa ya Assad kufanikiwa kuweka historia ya kuwa timu ya kwanza ya Kaunti ya Kwale kufuzu kushiriki ligi kuu.

Katibu wa Shirikisho la Soka Nchini (FKF) Kaunti ya Kwale, Shilingi Fumbwe, pamoja na mwakilishi wa soka ya wanawake tawi hilo Fatma Mwinyi wana hamu kubwa kwa Assad FC ifanikiwe kuweka historia, ya kuwa timu ya kwanza ya Kwale kufuzu kushiriki ligi kuu KPL.