Oscar Sudi aliteta kuwa William Ruto kwa sasa ametengwa na Rais Uhuru Kenyatta licha ya juhudi zake za kuomba kura kwa serikali ya Jubilee 2018. Picha: State House Source: Facebook
“Kwa sababu mimi na Uhuru Kenyatta, Raila Odinga na Musalia Mudavadi na wengine tunafanyaga kazi lakini jioni tunaweza fika mahali tukunywe glasi ya kileo. Lakini Ruto alifanya kazi usiku na mchana,” alisema Sudi.
Mbunge huyo aliwataka Wakenya kumuunga mkono DP akisema siasa za 2022 zitakuwa kati ya
Mbunge huyo alisema watahakikisha wamekoroga chama cha Jubilee kabla ya kuondoka. Picha: Oscar Sudi Source: UGC
“Hustler nation sio mzaha, ni lazima tutenganishe mafuta na maji katika taifa la Kenya ili kila mtu akae akijua Kenya hii hakuna asiye na lake,” aliongeza Sudi.
Alimtaka katibu wa Jubilee Raphael Tuju kutoa hesabu ya jinsi fedha za chama zimekuwa zikitumika.
“Kabla ya nyinyi kufukuza Caleb (naibu katibu wa Jubilee) tunataka tujua jinsi fedha zetu zimekuwa zikitumika. Na sisi si viwete, hatutatoka tu hivi tuende, tutakuwa tumeshikana mashati ndio mjue ata sisi ni wanaume,” alisema Sudi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.