Connect with us

General News

Team Kenya yamaliza Riadha za Dunia za Ukumbini katika nambari ya 22 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Team Kenya yamaliza Riadha za Dunia za Ukumbini katika nambari ya 22 – Taifa Leo

Team Kenya yamaliza Riadha za Dunia za Ukumbini katika nambari ya 22

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya Kenya imeratibiwa kurejea nyumbani Jumanne kutoka Belgrade, Serbia ambako ilikokamilisha Riadha za Dunia za Ukumbini katika nafasi ya 22 kati ya zaidi ya mataifa 130 yaliyoshiriki mnamo Machi 18-20.

Mshindi wa nishani ya shaba ya Riadha za Dunia za chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mbio za mita 800 Noah Kibet alishindia Kenya medali yake ya kwanza Machi 19. Abel Kipsang alizoa nishani ya shaba katika mbio za mita 1,500 Machi 20.

Kenya iliwakilishwa na wanariadha 10 akiwemo mshikilizi wa rekodi ya Afrika mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala aliyebanduliwa katika nusu-fainali ya mbio za mita 60.

Kenya ilivuna medali moja ya shaba kupitia kwa Bethwell Birgen katika Riadha za Dunia za Ukumbini nchini Uingereza mwaka 2018 ikimaliza katika nafasi ya 24.

Katika makala ya 2021, Ethiopia ilinyakua taji kwa medali nne za dhahabu, tatu za fedha na mbili za shaba ikifuatiwa na mabingwa wa miaka nyingi Amerika (dhahabu tatu, fedha saba na shaba tisa), Ubelgji (dhahabu mbili), Uswisi (dhahabu moja na fedha mbili) na Uswidi (dhahabu moja, fedha moja na shaba moja) katika nafasi tano za kwanza duniani. Kenya, ambayo iliwakilishwa na wanariadha 10, ilikuwa ya pili barani Afrika na nambari 22 duniani kwa medali moja ya fedha na moja ya shaba. Nigeria (fedha moja) na Uganda (shaba moja) zinakamilisha orodha ya mataifa kutoka Afrika yaliyopata medali katika michezo hiyo inayofanyika kila baada ya miaka miwili.