Connect with us

General News

Tetu, eneobunge lisilochagua mbunge kwa mihula miwili – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Tetu, eneobunge lisilochagua mbunge kwa mihula miwili – Taifa Leo

Tetu, eneobunge lisilochagua mbunge kwa mihula miwili

NA REGINAH KINOGU

HUKU wanasiasa wakijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu, eneobunge la Tetu, Kaunti ya Nyeri limevutia wengi.

Kati ya wanasiasa waliojitokeza ni mbunge wa sasa James Gichui anayelenga kutetea wadhifa wake, Wachira Ngatia, Geoffrey Ndeto, mwaniaji wa 2017 Peter Kamuthu, Daniel Kimanyo, diwani mteule wa Nairobi Ann Thumbi na Grace Ngandu Kinaya ni kwamba tangu libuniwe mnamo 1988, hakuna mbunge ambaye amehudumu kwa mihula miwili na hilo sasa linampa mbunge wa sasa Bw Gichuhi wakati mgumu wa kutetea wadhifa wake.

Eneobunge la Tetu, liligawanywa kutoka Nyeri ya Kati na ni pana huku likianzia milima ya Aberdares upande wa juu hadi mito Gura na Sagana upande wa chini. Ina maeneo ya utawala (zoni) matatu; Muhoya, Thigingi (Tetu upande wa juu) na Aguthi (Tetu upande wa chini).

Marehemu Nahashon Kanyi Waithaka alihudumu kama mbunge wa kwanza wa Tetu kwenye uchaguzi wa 1988 na alikuwa kati ya mawaziri waliohudumu chini ya utawala wa Rais wa pili Mzee Daniel Arap Moi.

Alipoteza uchaguzi huo baada ya kubwagwa na Joseph Gethenji ambaye alisimama kwa tiketi ya DP.

Kabla ya kuchaguliwa mbunge, Bw Gethenji alihudumu kama Katibu wa Wizara ya Leba kwenye serikali ya Mzee Moi.

Mnamo 1997, Paul Gikonyo Muya alimbwaga Bw Githenji kabla ya kubanduliwa na Profesa Wangari Mathaai kupitia tiketi ya Narc mnamo 2002.

Profesa Maathai aliandikisha historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushinda tuzo ya hadhi ya Nobel kutokana na mchango wake katika kukuza demokrasia, amani na maendeleo.

Licha ya kung’aa na hata kutambuliwa kimataifa, Bi Mathai hakuchaguliwa tena mnamo 2007 kwa kuwa alipoteza kwa

Francis Nyammo aliyeshinda kwa tiketi ya PNU. Bw Nyammu naye alipoteza kwa Ndungu Githinji mnamo 2013. Bw Githinji alikuwa mwanawe Joseph Gethenji aliyehudumu kama mbunge wa pili wa eneo hilo.

Alijaribu kuvunja mtindo wa kutochaguliwa mara mbili mnamo 2017 lakini akatemwa nje na wakili James Gichuhi.

Hata hivyo, wakazi wanadai ukosefu wa uongozi bora ndio umekuwa ukisababisha wabadilishe wabunge. Inasemekana wengi wanasubiri kuona iwapo Bw Gichuhi atafanikiwa kuvunja mtindo wa muhula mmoja kwa kila mbunge hasa baada ya kuhama Jubilee kisha akajiunga na UDA.

“Sikuona haja ya kuwarejesha wabunge ambao niliwapigia kura mara ya kwanza kwa sababu hawakutimiza malengo yangu. Ingawa nilimpigia Bi Mathaai 2007, wengi walihisi rekodi yake ya maendeleo ilikuwa mbovu ndipo akashindwa,” akasema mkazi Simon Maina.