Connect with us

General News

Thika Engineers imepania kuibuka Ligi kuu msimu ujao – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Thika Engineers imepania kuibuka Ligi kuu msimu ujao – Taifa Leo

Thika Engineers imepania kuibuka Ligi kuu msimu ujao

Na JOHN KIMWERE

TIMU ya wana Jeshi ya Thika Engineers ni kati ya vikosi vya handiboli ya wanaume vinavyopania kujituma mithili ya mchwa kwenye ngarambe ya Ligi Kuu muhula ujao.

Timu hiyo yenye makazi yake katika kambi la jeshi mjini Thika ambayo imekuwa chini ya kocha, Benjamin Wanje kwa sasa inalenga kupambana mwanzo mwisho kwenye kuhakikisha inatimiza azma ya kumaliza kati ya tano bora. ”Bila kujisifia tumejiwekea malengo tofauti kinyume na miaka iliyopita.

Tunataka kukabili wapinzani wetu wakiwamo mafahali wa mchezo huo Halmashauri ya Nafaka na Mazao nchini (NCPB),” kocha` wake, Albert Mukoya Murunga alisema na kuongeza kuwa ili kutimiza azimio hilo itawabidi wazamie mazoezi makali ili kupata uzoefu kama wenzao.

SUPER CUP

Murunga amekuwa mchezaji wa kikosi hiki tangia mwaka 2005. Katika mpango mzima anadokeza kuwa ametwikwa jukumu la kukiongoza msimu uliyokamilika mwezi uliyopita. Anasema chini ya uongozi wake anataka kumaliza kati ya nafasi mbili ama tatu bora kwenye kampeni za msimu ujao.

Anashikilia kuwa kwa mara ya kwanza amegundua kwamba wachezaji wake wanatosha mboga kujituma na kujikatia tiketi ya kushiriki kipute cha shindano la Super Cup ambalo hushirikisha timu ambazo humaliza kati ya nafasi sita bora katika jedwali la Ligi Kuu.

Timu ya handiboli ya wanaume ya Thika Engineers…Picha/JOHN KIMWERE

Kwenye kampeni za ngarambe hiyo msimu uliyopita, madume hawa wa Thika Engineers walimaliza nafasi ya nane kwa kusajili alama 20, moja mbele ya Rangers.

KIPUTE CHA ECAHF

Katika kipute hicho, vijana wa NCPB chini ya kocha, Danston Eshikumo walihifadhi taji hilo kwa kubeba alama 34. Nao wanazuo wa Strathmore wake kocha Peter Mwathi waliridhika na nafasi ya pili kwa kusajili pointi 32, sawa na Black Mamba. Kenya General Service (GSU) iliibuka ya nne kwa alama 30, mbili mbele ya Ulinzi.

Wasomi wa chuo cha Kenyatta (KU) walifunga orodha ya vikosi vilivyonasa tiketi za Super Cup walipotia kapuni alama 24, moja mbele Buccaneers. ”Nasi pia tunatamani sana kushiriki mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (ECAHF) miaka ijayo,” nahodha wake, Cyrus Ongera alisema na kutoa wito kwa viongozi wao kutilia maanani hoja hiyo.

Nahodha huyo anapongeza timu za NCPB na Black Mamba kwa kuonyesha mchezo mzuri kwenye kampeni za ngarambe ya ECAHF inayokamilika leo jijini Dar es Salaam. Tanzania.

Anashikilia kuwa sekta ya spoti nchini inakabiliwa na ukosefu wa ufadhili hali ambayo huchangia washiriki wengi kuvunjika moyo. ”Ninashauri wachezaji wa michezo mbali mbali kujituma bila kulegeza kamba na kufahamu kuwa spoti ni ajira kama nyingine,” akasema.

Thika Engineers inajivunia kutawazwa mabingwa wa Ligi ya vikosi vya Wanajeshi nchini (KDF) muhula uliyopita. Pia mwaka 2019 ilifanikiwa kumaliza ya pili kwenye shindano la KDF Cup. Thika Engineers inajumuisha wachezaji kama: Kenneth Biwot, Hussein Khalif, Cyrus Ongera na Naffali Maina (nahodha na naibu wake), Lawi Kemei, Brian Mutunga, Samuel Waiganjo na Peter Mureithi.

Pia wapo Cliff Odoyo, Bonventure Kaduka, Dennis Mundara, Samuel Saningo, Felix Kariithi, Brian Mwinami na Wycliff Kinoti. Nao maofisa wa benchi la kiufundi wapo Benjamin Wanje, Fransicah Chepkemei na Moses Njau.

Timu ya handiboli ya wanaume ya Thika Engineers…Picha/JOHN KIMWERE

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending