Connect with us

General News

Toyota Kenya kusambaza magari 592 kwa polisi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Toyota Kenya kusambaza magari 592 kwa polisi – Taifa Leo

Toyota Kenya kusambaza magari 592 kwa polisi

Na LAWRENCE ONGARO

KAMPUNI ya kuunda magari ya Toyota Kenya, inatarajia kutoa jumla ya magari 592 ya aina ya Land Cruiser kwa idara ya polisi kwa lengo la kuhudumia wananchi.

Mnamo Ijumaa, mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Bw Arvinder Reel, alitoa magari 81 ya aina ya Land Cruiser kwa polisi.

Hafla hiyo iliyofanyika katika kampuni ya kuunda magari ya Kenya Vehicle Manufacturers (KVM) mjini Thika, ilihudhuriwa na mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw Martyn Broadfield, naibu mkuu wa polisi Bw Patrick Ndunda na afisa wa mauzo Bw Alex Munene.

Magari ya Toyota Kenya. Picha/ Lawrence Ongaro

Mkurugenzi wa kampuni ya Toyota Bw Reel, alisema ushirikiano wa serikali na kampuni hiyo ni muhimu kwa sababu magari hayo yatatumika hata katika sehemu kame kwani yanastahimili maeneo hayo.

“Tuna matumaini ya kwamba utendakazi wa polisi utakuwa mzuri kwa sababu magari hayo yatasambazwa katika kaunti zote nchini,” alisema Bw Reel.

Alisema ushirikiano wa serikali na kampuni ya Toyota Kenya ulianzishwa mwaka wa 2013 na tangu wakati huo, polisi wamekuwa na fursa nzuri ya kuwatumikia wananchi.

Alieleza kuwa baadhi ya magari yatakayosambazwa kote nchini ni aina ya LC76, na LC79 ambayo yote ni chapa Toyota Kenya, Land Cruiser.

Toyota Kenya inaunda Hilux single na Double Cab, Lori aina ya Hino, na mabasi.

” Tunafanya juhudi kuona ya kwamba tunaongeza kuunda magari mengi ya asilimia 40 kutoka asilimia 30,” akasema Bw Reel.

Alisema kulingana na uchunguzi wa kiuchumi uliofanyika mwaka huu wa 2021, mwaka jana 2020, kampuni ya Toyota ilifaulu kuunda jumla ya magari tofauti 7,725 akiahidi watafanya juhudi kuongeza idadi zaidi.

Anataja pia baadhi ya magari muhimu wanayounda kwa sasa na ambayo ni Toyota Hino, Suzuki, na Yamaha.

Toyota Kenya ina matawi mengine 31 kote nchini.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending