Connect with us

General News

Tupokee chanjo kulinda watoto dhidi ya maambukizi ya corona – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Tupokee chanjo kulinda watoto dhidi ya maambukizi ya corona – Taifa Leo

KINYUA BIN KINGORI: Tupokee chanjo kulinda watoto dhidi ya maambukizi ya corona

Na: KINYUA BIN KINGORI

Kwanza, Natumia safu hii kuwatumia wasomaji wa makala hii, Taifa Leo na Taifa Jumapili kwa jumla salamu za heri njema ya Krismasi kesho kutwa.

Visa vya corona vinazidi kuongezeka na kuna baadhi ya wazazi ambao wamekataa kupokea chanjo kwa visingizio visivyo na mbele wala nyuma.wanatumia uvumi kuwatia hofu hata watoto wao wanaotaka kuchanjwa.

Wakati serikali kupitia wizara ya afya imejitolea kuhakikisha imepata chanjo toshelezi kuhakikisha wananchi Usalama wao, kuna wazazi ambao hawaoni umuhimu wa juhudi hizo kwa kupuuza amri ya serikali kuwataka wananchi wote kuchanjwa.

Wakati huu wa likizo fupi ya Disemba, ambapo shule zote zimefungwa ni wajibu wa wazazi na jamii kujitolea kuhakikisha wamewaepushia watoto maambukizi ya corona kwa kuchanjwa na kuwapa hamasisho kuelewa umuhimu wa kuzingatia masharti yaliyowekwa kuzuia hatari ya kuenea kwa maradhi hayo kwa kuendelea kuvaa barakoa,kunawa mikono na kadhalika.

Inavunja Moyo kuona baadhi ya watu wakubwa ambao juhudi zao ndizo tu zinazoweza kufaulisha vita vya kupambana na maambukizi ya maradhi hayo hasa wakati huu kuna hofu ya kusambaa kwa Omicron wakionyesha kupuuza au kutojali hofu ya msambao wa maradhi hayo hatari.

Virusi vya Omicron vimethibitishwa nchini na ripoti ya shirika la afya Duniani (WHO) imetangaza vimesambaa katika mataifa 90 kote ulimwenguni.

Hivyo, inapaswa wazazi wawe mstari wa mbele kulinda watoto wao kipindi hiki kwa kuwazuia kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kusherehekea sikukuu ya Krismasi au mwaka mpya.

Tusihatarishe maisha ya watoto ambao ikiwa wataambukizwa maradhi hayo huenda wataambukiza wenzao shule zikifunguliwa majuma mawili yajayo na kuchangia ongezeko la maambukizi hayo na kusababisha masomo kote nchini kuvurugwa ikiwa shule zitafungwa kutokana na maambukizi ya covid 19 au Omicron.

Serikali kushirikiana na machifu na wazee wa mitaa inafaa ianzishe misako mikali vijijini na mjini kuwatambua wananchi ambao wamepuuza agizo la kuchanjwa. Watakaogunduliwa hajachanjwa wapewe chanjo hiyo,na wale watakaotatiza kwa kukataa wachukuliwe hatua .

Hadi sasa hakuna dawa ya homa hiyo hatari imethibitishwa na WHO na chanjo ndiyo pekee inayoweza kuzuia msambao,na watu wasipochanjwa kwa ujeuri wao itakuwa sawa na kutishia maisha ya wengine hasa watoto ambao huenda hawana ufahamu juu ya hatari ya maradhi hayo.

Tujihadhari msimu huu wa sherehe tujiepushe na maambukizi ya covid 19 kwa kuhakikisha kila mmoja wetu katika jamii anaelewa kuhusu umuhimu wa kuzingatia masharti yaliyowekwa kuzuia hatari ya kuenea kwa maradhi hayo ikiwemo kupokea chanjo.