Connect with us

General News

TUSIJE TUKASAHAU – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

TUSIJE TUKASAHAU – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU

TUME ya Kukadiria Mishahara ya Watumishi wa Umma (SRC) imependekeza nyongeza ya mishahara na marupurupu ya viongozi waliochaguliwa wakiwemo wabunge na madiwani.

Kwa mfano, katika mapendekezo yaliyotolewa Jumanne, SRC inapendekeza kuongeza mshahara wa wabunge na maseneta kwa kiwango cha asilimia 14, kutoka Sh621,250 hadi 710,000. Nyongeza hiyo itaanza kutekelezwa kati ya miaka ya kifedha ya 2021/2022 na 2022/2023.

Lakini mwenyekiti wa tume hiyo, Bi Lyn Mengich asije akasahau kuwa mnamo Juni mwaka huu, kwenye kikao na wanahabari katika hoteli ya Hilton, Nairobi alitangaza kusitishwa kwa nyongeza zozote za mishahara kwa watumishi wa umma na maafisa wa serikali hadi mwaka wa 2023.

Alisema hatua hiyo itaathiri walimu na maafisa wakuu wa serikali, ambao wanajumuisha wabunge, madiwani na majaji.Bi Mengich alisema SRC ilisitisha nyongeza ya mishahara kutokana na athari za Covid-19 kwa uchumi wa Kenya.

Mwenyekiti huyu asije akasau kuwa uchumi wa Kenya haujaimarika na ungali unatishiwa na kirusi kipya aina ya Omicron.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending