Connect with us

General News

Tutumie Kiswahili kukuza utangamano nchini Kenya – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Tutumie Kiswahili kukuza utangamano nchini Kenya – Taifa Leo

NGUVU ZA HOJA: Tutumie Kiswahili kukuza utangamano nchini Kenya

NA PROF JOHN KOBIA

KAMPENI za kisiasa zinapopamba moto nchini Kenya tunapokaribia uchaguzi mkuu mnamo Agosti 9, 2022, ni muhimu tutafakari dhima ya Kiswahili katika kukuza utangamano.

Lugha ni chombo kinachoweza kutumiwa kujenga au kubomoa taifa. Lugha ni ala inayoweza kutumiwa kuunganisha ama kutenganisha watu katika jamii.

Nchini Kenya, Kiswahili ni lugha ya taifa. Lugha ya taifa hutumiwa kuunganisha watu wa jamii mbalimbali ili kukuza utangamano. Kiswahili ni baraka na silaha ya uzalendo kwa Wakenya.

Wanasiasa wanapotafuta kura hutumia Kiswahili ili kushawishi wapigakura kutoka jamii mbalimbali kuwaunga mkono. Wanaweza kueleza sera na mipango yao kwa Kiswahili kwa sababu ni lugha inayotumiwa na watu wengi.

Tunapaswa kutumia Kiswahili kama jukwaa la kukwea mlima wa amani ili nchi iwe na utangamano na maendeleo kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi mkuu.

Lugha ya Kiswahili ikitumiwa vizuri ni chombo cha kukuza ushirikiano.

Kwa upande mwingine, lugha inaweza kutumiwa vibaya kupanda mbegu za chuki na uhasama miongoni mwa watu katika jamii.

Lugha ya Kiswahili ina utajiri wa methali, nahau, misemo, tashbihi, jazanda, misimu, taswira, mafumbo na msamiati ambao ukitumiwa vibaya unaweza kutatiza utangamano.

Ni muhimu kwa wanasiasa na wananchi kwa ujumla kutumia maneno kwa tahadhari kwa njia mwafaka kulingana na miktadha mbalimbali.

Maneno ya kawaida ya Kiswahili yanaweza kutumiwa katika muktadha wa kampeni za kisiasa na kuzua hofu na uhasama miongoni mwa watu. Tunapaswa kutumia maneno ya Kiswahili kwa uangalifu kulingana na miktadha mbalimbali.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending