Connect with us

General News

Ubabe wa Mvurya, Joho kuibuka upya – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ubabe wa Mvurya, Joho kuibuka upya – Taifa Leo

Ubabe wa Mvurya, Joho kuibuka upya

NA SIAGO CECE

USHINDANI wa ubabe wa kisiasa kati ya Gavana wa Mombasa, Bw Hassan Joho, na mwenzake wa Kwale, Bw Salim Mvurya, unatarajiwa kuibuka upya baada ya wawili hao kukwezwa kusimamia kampeni za urais za mirengo tofauti Pwani katika uchaguzi ujao.

Wawili hao walishirikiana katika Chama cha ODM kabla ya uchaguzi wa 2013 lakini Bw Mvurya akahamia Jubilee, chama ambacho alitumia kushinda uchaguzi uliopita baada ya kutofautiana na Bw Joho.

Katika uchaguzi ujao, Bw Joho anatarajiwa kuongoza kampeni za urais za Bw Odinga eneo la Pwani mbali na maeneo mengine ya nchi, huku Bw Mvurya akiwa katika upande wa Naibu Rais, Dkt William Ruto.

Kampeni za Bw Odinga zimekuwa zikiendelezwa chini ya Muungano wa Azimio la Umoja huku zile za Dkt Ruto zikiendeshwa kupitia kwa Kenya Kwanza.

Viongozi wa Kenya Kwanza, sasa wameanzisha juhudi za kumvumisha Bw Mvurya ili akubaliwe na Wapwani kuwa msemaji wao wa kisiasa katika ukanda huo.

Katika mkutano wa hadhara uliofanywa na muungano huo eneo la Lungalunga, Seneta wa Tharaka Nithi, Prof Kithure Kindiki, alitoa wito kwa jamii za Pwani kusimama wima na Bw Mvurya akisema ana uwezo wa kuwakilisha vyema matakwa yao katika meza ya siasa za kitaifa.

Kulingana naye, kuwepo kwa Bw Mvurya ndani ya kikosi kikuu cha Kenya Kwanza kunampa nafasi ya kushinikiza utekelezaji wa mipango itakayosaidia kutatua changamoto za eneo hilo endapo Kenya Kwanza itafanikiwa kushinda urais.

“Tunataka kuwahakikishia wakazi wa Pwani kuwa tutaketi na viongozi wenu wakiongozwa na Bw Mvurya ambaye atawawakilisha katika meza ya kitaifa. Tutajadili jinsi ya kufufua uchumi wa Pwani ambao umedorora,” Prof Kindiki akasema.

Bw Mvurya aliteuliwa kama kinara wa Kenya Kwanza mwezi uliopita wakati wa mkutano wa kisiasa Kwale ambapo Dkt Ruto alisema atachukua nafasi hiyo kuwakilisha eneo la Pwani.

Hivi majuzi, gavana huyo ambaye kwa sasa yuko katika ziara ya ng’ambo akiandamana na naibu rais, alifanya kikao na baadhi ya viongozi wanaoegemea upande wa naibu rais kupanga mikakati ya kutaka kuanzisha kampeni.

Viongozi wengine wa Pwani wanaotarajiwa kushirikiana naye ni aliyekuwa seneta wa Mombasa, Bw Hassan Omar, Naibu Gavana wa Kwale, Bi Fatuma Achani na wabunge wanaoegemea upande wa Dkt Ruto.

Kwa upande mwingine, Bw Joho anatarajiwa kushirikiana na magavana wa kaunti nyingine nne za Pwani pamoja na wabunge wanaoegemea muungano wa Azimio la Umoja wakiwemo wanachama wa Jubilee.

Prof Kindiki alikuwa akizungumza katika hafla ya kusherehekea Siku ya Wanawake Kwale ambapo aliandamana na viongozi wengine wa Kenya Kwanza akiwemo Seneta wa Bungoma, Bw Moses Wetang’ula.

Bw Wetang’ula alisema ana imani kuwa Dkt Ruto atashinda kura raundi ya kwanza, huku akimkosoa Rais Uhuru Kenyatta kwa kuingilia kampeni za urithi wake.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending