Connect with us

General News

Ubaguzi wa kijinsia waongezeka kwa asilimia 80 bungeni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ubaguzi wa kijinsia waongezeka kwa asilimia 80 bungeni – Taifa Leo

Ubaguzi wa kijinsia waongezeka kwa asilimia 80 bungeni

Na WINNIE ONYANDO

RIPOTI ya Muungano wa Mabunge Ulimwenguni (IPU) na Mabunge ya Afrika (APU) imebainisha kuwa ubaguzi wa kijinsia na unyanyasaji inapatikana kila mahali katika mabunge ya Afrika.

Ripoti hiyo ilibainisha kuwa asilimia 80 ya jinsia ya kike wanapokea dhuluma za kila aina bungeni. “Asilimia 67 ya wanawake wamebaguliwa bungeni. Asilimia 42 wamepokea vitisho vya mauaji, unajisi na vya kutekwa nyara. Asilimia 23 wamepitia dhuluma hizo katika njia moja au nyingine,” ikasoma ripoti.

Baadhi ya wanawake walioteuliwa au kuchaguliwa bungeni wamepokea dhuluma hizo kutoka kwa jinsia ya kiume hasa wale ambao ni wapinzani wao.

“Jinsia wa kike ambao ni wabunge na wanaishi na ulemavu, wanawake chini ya miaka 40, wanawake wasioolewa na wanawake kutoka vikundi vya wachache wanakabiliwa na matukio makubwa ya unyanyasaji. Wabunge wanaotetea haki za wanawake pia wanapitia dhuluma hizo.”

Rais wa IPU, Duarte Pacheco alisema kuwa ripoti hiyo imemulika janga la ubaguzi wa kijinsia katika mabunge ya Afrika.Alisema suala hilo sharti itatuliwe kwani inawanyima wanawake uhuru wa kujihusisha na masuala ya kisiasa.

“Hii itawafungia nje na kuwafanya wakate tamaa jinsia ya kike ambao ni vijana na wanataka kujiunga na masuala ya kisiasa.” Kwa upande wake, Rais wa APU, Mohamed Ali Houmed alisema mabunge yanapaswa kuwachukulia hatua watu wanaowadhulumu wanawake.

“Ni jukumu la taasisi zetu na wabunge wote, wanaume na wanawake, kuchukua hatua za haraka ili kumaliza ubaguzi wa kijinsia.” Naye Naibu Rais wa IPU, Adji Diarra Mergane Kanouté alitoa wito wa ushirikiano ili kumaliza ubaguzi wa kijinsia ulimwenguni.

Ripoti hiyo pia ilionyesha kuwa wabunge ambao ni jinsia ya kike wanaotoka katika nchi za Afrika wanapitia dhuluma za kimapenzi ikilinganishwa na wanaotoka Ulaya. “Hakuna usalama bungeni. Asilimia kubwa za dhuluma hutokea bungeni. Tunafaa kuwapa jinsia ya kike mazingira yenye usalama ili waweze kufanya kazi bila uwoga,” akasema Bw Houmed.

Viongozi hao walipendekeza kuwa kila serikali iweke sera za ndani za bunge ili kukabiliana na ubaguzi wa kijinsia, kuanzisha maeneo ya siri ambapo waathirika wanaweza kupata ushauri na uundaji wa mifumo ya kupokea na kushughulikia malalamishi ambayo ni huru, salama na ya haki.