Connect with us

General News

Ubaguzi wa rangi ungalipo na Mwafrika ndiye mhanga mkuu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ubaguzi wa rangi ungalipo na Mwafrika ndiye mhanga mkuu – Taifa Leo

DOUGLAS MUTUA: Ubaguzi wa rangi ungalipo na Mwafrika ndiye mhanga mkuu

NA DOUGLAS MUTUA

UBAGUZI wa rangi ni tatizo lisiloweza kutabirika litaisha lini. Kila unapofikiri watu wamekuwa wastaarabu na hawabaguani tena kama mwanzo, mapya yanazuka.

Vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine vimetukumbusha mambo mawili: Ubaguzi wa rangi haujaisha, na Mwafrika angali mhanga mkuu wa tatizo hilo.

Video zimeibuka mtandao – ni zikionyesha Waafrika, hasa wanafunzi wanaosoma Ukraine, wakizuiwa kuabiri magari ya moshi ili kutoroka eneo la vita.

Ipo iliyoonyesha Waafrika wakisukumwa kama magunia ya makaa au viazi; nadhani hata ukisukuma makaa unakuwa mwangalifu usiyavunjevunje, viazi navyo huvipondi vikiwa vibichi.

Hiyo inaweza kutolewa kisingizio kwamba, katika hali ya mguu niponye, chochote kinaweza kutokea na hivyo basi anayemsukuma mtu hajali rangi ya anayesukuma. Hata hivyo, ipo video nyingine iliyoudhi zaidi ambapo wenyeji, raia wa Ukraine, walishikana mikono na kubiza mlango wa gari moshi ili Waafrika wasiabiri! Hiyo ni ithibati kwamba,

waliaminia na kukusudia kuwaweka watu weusi hatarini; wenyeji hao wangekuwa hatarini, nia yao iwe tu ni kujinusuru, hawangeungana kuwazuia binadamu wenzao. Hiyo ni ithibati kwamba, nia yao kuu ilikuwa kuhakikisha weusi hao wameangamia kwa vyovyote vile, ndiposa wakajaribu kuwaweka pale ili hatari itoke itokako na kuwapata.

Video nyingine ya kuudhi ilionyesha watu weusi waliokimbia vita hivyo wakizuiwa kuvuka mpaka na kuingia Ukraine ilhali wazungu wakinyakuliwa na kuokolewa kutoka hatari hiyo.

Sheria za kimataifa, ambazo Urusi inakumbushwa tena na tena kwamba imekiuka, zinamtetea na kumlinda sana mkimbizi kwa kuwa inaaminika hakimbii kwa raha zake. Yeyote anayemzuia kukimbia ni msaidizi na mwezeshaji katika kadhia nzima iliyomweka hatarini mtu anayekimbia.

Wakuu wa Muungano wa Uropa (EU) walipolalamikiwa kwamba, mataifa wanachama ambayo yanapakana na Ukraine yanaendeleza ubaguzi walikanusha habari hizo hata kabla ya kuzichunguza.

Walisisitiza yeyote anayekimbia Ukraine, bila kujali rangi yake, yuko radhi kwenda kokote katika mataifa wanachama wa Muungano huo katika muda wa siku 90.

Baada ya muda huo, itachukuliwa kwamba taifa atakalokuwa mtu wakati huo ndilo alilochagua kuwa makao yake mapya kama mkimbizi.

Unalofaa kujua ni kwamba, wabaguzi wa rangi ni wagonjwa wa akili, na ni kosa kubwa kumchukia mtu mgonjwa. Muhimu ni kumpenda na kutotarajia hisani yoyote kwake. Hivyo ndivyo tutakavyoibadilisha dunia.

[email protected]

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending