Connect with us

General News

Uchaguzi mdogo Ukambani wampa Ruto ujasiri – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Uchaguzi mdogo Ukambani wampa Ruto ujasiri – Taifa Leo

Uchaguzi mdogo Ukambani wampa Ruto ujasiri

Na PIUS MAUNDU

MATOKEO ya Uchaguzi Mdogo wa Wadi ya Nguu/Masumba, Kaunti ya Makueni, yamempa Naibu wa Rais William Ruto ujasiri na matumaini ya kupata kura kwa wingi katika eneo la Ukambani 2022.

Dkt Ruto alipiga kambi katika Kaunti ya Makueni kwa siku tatu wiki iliyopita.

Jumamosi, Dkt Ruto alihudhuria hafla ya kusherekea matokeo ya aliyekuwa mwaniaji wa chama cha United Democratic Alliance (UDA), Daniel Musau.

Bw Musau aliibuka katika nafasi ya pili nyuma ya Timothy Maneno, mwaniaji wa kujitegemea.

Mwaniaji wa Wiper, Eshio Mwaiwa alikuwa wa tatu – hali ambayo imefasiriwa kuwa ni kushuka kwa umaarufu wa kinara wa chama hicho Kalonzo Musyoka katika eneo la Ukambani.

Dkt Ruto anaamini kwamba matokeo hayo ya uchaguzi mdogo yalikuwa ishara kwamba anakubalika katika eneo la Ukambani na huenda akajipa maelfu ya kura katika eneo hilo mwaka ujao.

“Japo hatukushinda kiti cha Nguu/Masumba, tulishinda Wiper. Nimekuja hapa kuwashukuru kwa kupigia UDA kura kwa wingi. Naamini mtaendelea vivyo hivyo hadi tuunde serikali ijayo,” akasema Dkt Ruto alipokuwa akihutubu mjini Matuu.

Naibu wa Rais aliyekuwa ameandamana na Seneta wa Kajiado Philip Salau na wabunge Victor Munyaka (Machakos Mjini), Aden Duale (Garissa Mjini) na Rigathi Gachagua (Mathira), alipigia debe mpango wake wa bottom up ambao anadai utaangamiza umaskini nchini.

Eneo la Ukambani lina kura milioni 1.6 na kila mwaniaji wa urais anataka kumega sehemu katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Kiongozi wa ODM Raila Odinga ambaye ameonyesha dalili za kuwania urais mwaka ujao, anaonekana kutishia umaarufu wa Dkt Ruto katika eneo la Ukambani.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending