Connect with us

General News

UDA kuiga IEBC kuandaa uteuzi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

UDA kuiga IEBC kuandaa uteuzi – Taifa Leo

UDA kuiga IEBC kuandaa uteuzi

GITONGA MARETE NA ALEX NJERU

CHAMA UDA kinachoongozwa na Naibu Rais Dkt William Ruto sasa kinapanga kuiga mfumo unaotumika na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini (IEBC) wakati wa uchaguzi mkuu, kuandaa uteuzi wake kati ya Aprili 9 na Aprili 16.

Mwenyekiti wa Bodi ya Uchaguzi (NEB) Anthony Mwaura alifichua ku – wa, watawaajiri makarani, kutumia masanduku ya kupigakura yenye nembo maalum ya kiusalama ikizingatiwa

mchujo huo utakuwa wenye ushindani mkali hasa maeneo chama hicho kinajivunia wafuasi wengi.

Bw Mwaura alikariri kuwa uteuzi huo utakuwa huru na haki akiwa ziarani kaunti za Mlima Kenya.

Wakati wa ziara hiyo, alikutana na wawaniaji kutoka kaunti za Isiolo, Marsabit, Wajir, Mandera, Meru, Tharaka Nithi, Embu na Kirinyaga. Leo atakutana na wawaniaji katika kaunti za Nyeri na Murang’a.

Kumekuwa na madai kuwa UDA imeamua kuwapa baadhi ya wawaniaji tiketi za moja kwa moja. Hata hivyo, Bw Mwaura aliyapuuza madai hayo aliyoyasema si kweli na akasisitiza kuwa, uteuzi utakuwa huru na wa haki kwenye viti vyote sita vinavyowaniwa.

“Tulifika hapa kushauriana na wawaniaji, kuyashughulikia masuala

wanayoibua na pia kuwahakikishia kuwa uteuzi wa chama utakuwa huru na wa haki mwezi ujao. Ni mshindi wa uteuzi huo atatangazwa kupeperusha bendera kwenye kila wadhifa unaowaniwa,” akasema Bw Mwaura mjini Meru.

Bw Mwaura alionyesha imani yake kuwa UDA itawalemea wapinzani wao eneo la Mlima Kenya, akisema umaarufu wa Dkt Ruto bado u mbali sana na kamwe hawezi kufikiwa na kinara wa ODM Raila Odinga ambaye ndiye mpinzani wake mkuu.

“Kwa muda wa miaka minne iliyopita, Naibu Rais ametembelea Meru mara 55 ilhali wapinzani wetu Jubilee wametembelea eneo hili mara tano pekee. Hawajali kuhusu wapigakura ila wao huja tu kusaka kura uchaguzi mkuu unapokaribia,” akaongeza.