Connect with us

General News

Ufanyeje kukabili maumivu kwenye tupu ya nyuma? – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ufanyeje kukabili maumivu kwenye tupu ya nyuma? – Taifa Leo

JIJUE DADA: Ufanyeje kukabili maumivu kwenye tupu ya nyuma?

NA PAULINE ONGAJI

WANAWAKE wengi hukumbwa na tatizo la maumivu kwenye tupu ya nyuma mara kwa mara, suala linalowaingiza baridi.

Maumivu haya yaweza tokana na jeraha (anal fissure), linalosababishwa hasa mhusika anapoenda choo kikubwa au kigumu. Aidha, hali hii yaweza sababishwa na hemorrhoids (kuvimba kwa mishipa ya damu kwenye sehemu ya tupu ya nyuma).

Pia, yaweza sababishwa na nasuri ya tupu ya nyuma, misuli kujivuta, maambukizi, kuendesha, kidonda au kansa.

Unapokumbwa na hali hii unahimizwa kumuona daktari ili ufanyiwe uchunguzi wa kina. Tiba hutegemea na nini hasa kinachosababisha hali hii.

Waweza zuia tumbo kuvimba na kinyesi kuwa kigumu kwa kunywa maji mengi, kula chakula kilicho na kiwango cha juu cha nyuzi, kufanya mazoezi na kuwa na ratiba ya kuenda haja kubwa.

Pia, waweza kaa kwenye beseni yenye maji yaliyopashwa moto kwa angaa dakika 20 kila siku ili kusaidia kutuliza tishu iliyojeruhiwa.

Kuna vijalizo vya nyuzi pia ambavyo vyaweza kusaidia kupitisha choo chepesi.