Connect with us

General News

Ugavana wa Nairobi mtihani kwa Azimio – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ugavana wa Nairobi mtihani kwa Azimio – Taifa Leo

Ugavana wa Nairobi mtihani kwa Azimio

NA COLLINS OMULO

RAIS Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, wanakabiliwa kibarua kigumu kubuni mwafaka miongoni mwa wawaniaji wanaolenga kugombea nafasi za kisiasa katika Kaunti ya Nairobi chini ya vuguvugu la Azimio la Umoja.

Viongozi hao, ambao wamekuwa wakifanya kazi pamoja baada ya handisheki mnamo Machi 9, 2018, wametangaza mpango wa kufanya mchujo wa pamoja chini ya vuguvugu hilo uchaguzi wa Agosti unapokaribia.

Wanashikilia hatua hiyo itaongeza uwezekano wa vuguvugu hilo kujizolea kura nyingi na viti vingi jijini Nairobi.

Hata hivyo, wanakabiliwa na mtihani kuhusu jinsi ya kutimiza matakwa ya kisiasa ya jamii tofauti, kwenye juhudi za kubuni mikakati kukabili muungano wa Kenya Kwanza Alliance (KKA).

Muungano huo unawashirikisha Naibu Rais William Ruto chini ya chama cha UDA, Bw Musalia Mudavavi (ANC) na Seneta Moses Wetang’ula (Ford-Kenya).

Wagombeaji wawili—Seneta Johnson Sakaja na aliyekuwa mbunge wa Starehe, Bi Margaret Wanjiru—wamejitokeza kama wagombea wakuu wanaotafuta uungwaji mkono wa muungano huo katika nafasi ya ugavana.

Chini ya mkataba wa vyama vya Jubilee na ODM, imeibuka mgombea wa ugavana atatoka katika Jubilee (eneo la Mlima Kenya) huku mgombea-mwenza wake akitoka katika ODM.

Hata hivyo, kambi mbili za kisiasa tayari zimeibuka katika vuguvugu hilo, ambapo zote zinadai kuwa na ukaribu kutoka kwa viongozi hao wawili.

Ni hali ambayo imetabiriwa kuzua ushindani mkali wa kisiasa, kando na kutishia umoja ulio katika vuguvugu hilo. Kambi moja inamuunga mkono mbunge Tim Wanyonyi (Westlands) kuwa gavana, huku kambi nyingine ikimhusisha kiongozi wa Chama cha Wenye Biashara Kenya (KNCCI), Bw Richard Ngatia.

Kambi ya Bw Wanyonyi inawajumuisha Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna, aliyekuwa mbunge wa Dagoretti Kusini Dennis Waweru na Mwakilishi wa Kike katika Kaunti ya Nairobi, Bi Esther Passaris.

Kambi ya Bw Ngatia inawajumuisha Mbunge Maalum Maina Kamanda, mbunge George Aladwa (Makadara) na Seneta Maalum Beatrice Kwamboka.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending