Connect with us

General News

Uhaba wa ngano wanukia wakulima wakisusia kilimo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Uhaba wa ngano wanukia wakulima wakisusia kilimo – Taifa Leo

Uhaba wa ngano wanukia wakulima wakisusia kilimo

NA BARNABAS BII

HUENDA Kenya ikakabiliwa na uhaba wa ngano huku wakulima zaidi wakitishia kuacha kilimo cha zao hilo.

Wakulima wanaishutumu serikali kwa kujaza soko na nafaka ya bei ya chini inayoagizwa nchini kutoka mataifa ya kigeni hatua inayowasababishia hasara wakulima wa humu nchini.

Wataalam wa masuala ya kilimo na uchumi wamelalamikia kuongezeka kwa gharama ya uzalishaji kutokana na kupanda kwa bei za mbolea, mbegu, dawa za kunyunyizia wadudu, ambazo zimewalazimu wakulima kupunguza ekari wanazotumia kukuza zao hilo.

“Imekuwa hatari mno kuwekeza katika kilimo cha ngano kutokana na hali ya anga isiyotabirika, mikurupuko ya maradhi inayozuka na bei za soko zinazobadilika kila mara,” alisema Bw David Sang, kutoka Sergoit, Kaunti Uasin Gishu.

Eneo la Bonde la Ufa lilitoa jumla ya magunia 4.5 milioni ya ngano kutoka hektari 127,825 za ardhi zilizopandwa msimu uliopita.

Kenya huzalisha jumla ya tani 365,600 dhidi ya kiwango kinachotumiwa cha tani 8.4 milioni hivyo kuilazimu nchi kuagiza kiasi kinachosalia kutoka nje ya nchi.

Ardhi inayotumiwa kwa ukuzaji wa ngano imepungua katika Kaunti ya Uasin Gishu kutoka hektari 40,000 hadi hektari 18,000 huku wakulima wakigeukia aina nyingine ya kilimo kama vile ufugaji wa ng’ombe wa maziwa.

“Kiasi cha ardhi inayokuziwa ngano kimepungua pakubwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita hali ambayo imeathiri vibaya ulaji na bei ya bidhaa za ngano,” alisema Bw Samuel Yego, waziri wa kilimo wa Kaunti hiyo.

Idadi kubwa ya viwanda vinanunua zao hilo kwa Sh4,200 kwa kila gunia ya kilo 90 bei ambayo wakulima wanasema ni duni ikilinganishwa na gharama ya uzalishaji.

“Ukuzaji wa ngano ni shughuli inayohitaji nguvu na kugawanya ardhi katika vipande vidogo vidogo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu hali inayofanya kilimo cha zao hilo kuwa cha hasara,” alisema Bw Wilson Kosgei, mkulima wa ngano kutoka Moiben, Kaunti ya Uasin Gishu.

“Wakulima eneo hili wanaendelea kukuza ngano ya kiwango bora zaidi ikilinganishwa na kile viwanda wanachoagizia kutoka nje hali ambayo imewavunja moyo kuhusu kuwekeza katika zao hilo,” alisema. Wakulima wa ngano wameelezea hofu ya kukwama kutokana na mikurupuko ya kila mara ya magonjwa ya ngano na sasa wanataka teknolojia mpya zianzishwe ili kuongeza uzalishaji na kuwaletea mapato bora.

“Kando na kutumia teknolojia mpya, wakulima wa ngano wanahitaji mbegu bora za kiwango cha juu zinazoweza kustahimili mabadiliko ya hali ya anga,”alisema

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending