Connect with us

General News

Uhuru aandikiwa barua kuhusu mauaji Kerio – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Uhuru aandikiwa barua kuhusu mauaji Kerio – Taifa Leo

Uhuru aandikiwa barua kuhusu mauaji Kerio

NAIBU Gavana Elgeyo Marakwet Wisley Rotich amemwandikia barua ya malalamishi Rais Uhuru Kenyatta kuhusu anachokitaja kama “msururu wa mauaji yanayoendelea katika Bonde la Kerio ambayo huenda yakasababisha kuangamia kwa jamii.”

Katika barua yake ya kurasa nne, Bw Rotich alisema kukithiri kwa mashambulizi yasiyodhibitiwa yanayotekelezwa na majangili, kupoteza maisha na mali ikiwemo kujikokota kwa serikali kuchukua hatua, kulimchochea kumwandikia barua moja kwa moja Kiongozi wa Taifa akimwomba kuingilia kati.

“Pia nimependekeza suluhisho za muda mfupi na muda mrefu kuhusu jinsi tunavyoweza kukabiliana na kero la majangili kwenye ukanda wa Bonde la Kerio. Ni matumaini na ombi langu kuwa Rais atasikiza kilio chetu,” Naibu Gavana alieleza Taifa Leo.

“Wakati Luteni Jenerali (mstaafu) Roméo Dallairb aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha UN kwenye Oparesheni Nchini Rwanda (UNAMIR) alipoondoka Rwanda baada ya mauaji ya halaiki alijutia baadhi ya makosa ya UN ambayo yangezuia vifo vya watu 800,000 katika muda wa siku 100, aliandika Naibu Gavana.

“Baadaye aliandika kitabu chenye anwani ‘Shaking hands with the Devil’ baada ya kukabiliana na mshtuko mnamo 2001,” alieleza.