Connect with us

General News

Uhuru atetea hatua yake kuelekeza baadhi ya taasisi, mashirika kusimamiwa na idara ya jeshi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Uhuru atetea hatua yake kuelekeza baadhi ya taasisi, mashirika kusimamiwa na idara ya jeshi – Taifa Leo

Uhuru atetea hatua yake kuelekeza baadhi ya taasisi, mashirika kusimamiwa na idara ya jeshi

NA SAMMY WAWERU

RAIS Uhuru Kenyatta ametetea hatua yake kugeuza baadhi ya taasisi na mashirika ya serikali kuongozwa na maafisa wa jeshi, KDF.

Kiongozi wa nchi amesema uamuzi huo ulichochewa na ufujaji wa mali ya umma, ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi, katika mashirika hayo.

Amesema Jumatano, wakati wa maadhimisho ya Madaraka Dei, Makala ya 59, kikosi cha jeshi kimeonyesha uwazi katika utendakazi wake.

“Baadhi wamenikosoa kwa uamuzi huo, ila nawajibu Kenya ni nchi yenye demokrasia na tutafanya mambo ambayo yatatufaa kama taifa,” Rais Kenyatta akasema.

Akaendelea kueleza: “Sitasita kutumia maafisa wa kijeshi kurekebisha sehemu ambazo wengine walishindwa.”

Shirika la nyama nchini, ndilo Kenya Meat Commission (KMC), ni baadhi ya taasisi za serikali zinazoongozwa na maafisa wa KDF.

Mwaka 2020, Rais Kenyatta alikabidhi kikosi cha jeshi KMC, hatua ambayo ilikosolewa na wapinzani wake.

“Chini ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya kukabidhiwa, waligeuza KMC kuwa shirika linaloingiza faida ya kuridhisha,” akasema.

Alisema, awali kabla ya uamuzi huo, lilikuwa likikadiria hasara hivyo basi kukosa kuwafaa wafugaji nchini.

Shirika la Kustawisha Jiji la Nairobi (NMS), pia linaongozwa na maafisa wa jeshi.