Connect with us

General News

Uhuru azindua usambazaji wa mlo maeneo kame – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Uhuru azindua usambazaji wa mlo maeneo kame – Taifa Leo

Uhuru azindua usambazaji wa mlo maeneo kame

NA PSCU

RAIS Uhuru Kenyatta jana Jumatatu alizindua shehena ya chakula cha msaada kitakachosambazwa katika kaunti 23 zinazokabiliwa na ukame.

Kulingana na Ikulu, msaada huo utafaidi Wakenya milioni 2.3 katika kaunti hizo.

Kiongozi wa Taifa alikariri kwamba serikali inalenga kutekeleza mipango ambayo itajenga ustahimilivu katika familia zisizojiweza, kuimarisha maisha kupitia shughuli zinazoathiriwa na ukame, zinazostahimili ukame na vile vile kuimarisha mifumo ya kutoa tahadhari mapema na ubashiri wa hali ya anga.

Rais Kenyatta alisema kutoka Oktoba 2021 hadi leo, jumla ya ng’ombe 11,250 na mbuzi na kondoo 3,200 wamenunuliwa na kiwanda cha KMC kutoka kwa wafugaji katika kaunti zilizoathiriwa zaidi na ukame.

Rais Kenyatta alisema serikali yake kupitia Vikosi vya Ulinzi imejenga vituo 10 vya maji pamoja na visima vitatu katika Kaunti ya Marsabit, vituo vitatu pamoja na visima vitatu vya maji katika kaunti za Laikipia na Baringo.

ili kupunguza mzigo kwa jamii zinazoishi katika maeneo kame.

“Visima hivyo vimekamilika pamoja na kazi husika kwa matumizi ya nyumbani na mifugo. Kwa sasa, tunapanua mpango huo kushughulikia kaunti ya Wajir, Mandera, Garissa, Tana River, Meru, na sehemu za Machakos na Kitui,” akasema Rais.

Wakati huo huo, Rais aliagiza wizara husika pamoja na mashirika kupiga jeki kwa haraka mpango wa marupurupu ya pesa kupitia usambazaji wa vyakula vya msaada ili kukabiliana na changamoto kama vile familia zinazokabiliwa na hatari ambazo hazina rununu na vifaa.

“Aidha naagiza wizara husika pamoja na mashirika kuhakikisha kwamba mipango ya kufufua ufugaji, mpango wa maji, pamoja na msaada wa vifaa vya matibabu na vyakula vya msaada vinafikia watu wanaoathirika katika kaunti hizi bila kuchelewa,” akasema Rais.

Aliwapongeza washikadau wote zikiwemo serikali za kaunti, mashirika ya kutoa misaada na washirika wa maendeleo kwa kusaidia mikakati ya serikali ya kitaifa ya kukabiliana na kiangazi.

Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Martin Wambora ambaye pia ni Gavana wa Kaunti ya Embu na mwenzake wa Mandera Ali Roba ambaye vile vile ni Mwenyekiti wa kaunti za maeneo kame nchini walimpongeza Rais Kenyatta pamoja na serikali ya kitaifa kwa kuingilia kati kusaidia kaunti hizo ambazo zimekabiliwa na kiangazi.

“Mheshimiwa, niruhusu kuipongeza serikali ya kitaifa chini ya usimamizi wako bora kwa kuendelea kusaidia kaunti za maeneo kame hususan wakati huu mgumu ambapo tunakabiliwa na athari na matatizo ya kimazingira,” akasema Gavana Wambora.

Mkuu wa Utumishi wa Umma Dkt Joseph Kinyua, Waziri wa Usalama wa Ndani Dkt Fred Matiang’i na wakilishi wa magavana kutoka kaunti zinazoathirika na kiangazi walihudhuria sherehe hiyo fupi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending