Connect with us

General News

Ukitaka kuvuna vinono kutokana na ufugaji wa ndege, tambua mahitaji ya soko – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ukitaka kuvuna vinono kutokana na ufugaji wa ndege, tambua mahitaji ya soko – Taifa Leo

Ukitaka kuvuna vinono kutokana na ufugaji wa ndege, tambua mahitaji ya soko

Na SAMMY WAWERU

MRADI wa ufugaji wa ndege wa umaridadi anaoendeleza Peter Kimani alianza kuufanyia kazi mwaka 2016, kama njia mojawapo ya kujipa pato la ziada.

Alichukua hatua hiyo kutokana na mshahara aliolipwa akiutaja “kuwa kiduchu”.

Kimani alikuwa mhasibu, katika kampuni moja jijini Nairobi.

Ni hali inayokumba wengi, gharama ya matumizi nyumbani hasa mahitaji muhimu ya kimsingi; chakula, matibabu, elimu, mavazi na nauli kuelekea wanakozimbulia mkate wa kila siku ikizidi kwa kiwango kikubwa mshahara.

Gurudumu la maisha lazima lisukumwe, liwalo na liwe.

Chaguo la kukumbatia ufugaji wa ndege maridadi, kulingana na Kimani ni la busara na asilojutia kamwe.

Ukiwa katika mtaa wenye shughuli tele za kibiashara, Umoja, mazingira pana ya Kaunti ya Nairobi, mradi wake una mseto wa ndege, kuanzia kanga wenye madoadoa meusi na meupe na wale weupe, bata bukini, bata mzinga na njiwa.

Isitoshe, hufuga bata aina ya Pekins, Rouen, Silkie bantams (kuku mdogo na maridadi), Egyptian runners na kuku wa kienyeji.

“Mradi huu ndio afisi yangu ya kila siku,” akaambia Akilimali wakati wa mahojiano.

Akionekana kuwa mwingi wa furaha, Kimani ambaye ni baba wa watoto wawili alisema familia yake anaikimu riziki kupitia ufugaji anaoendeleza, pamoja na miradi mingine iliyozaliwa kupitia mapato ya ndege.

Aidha, umemfanikisha kufungua biashara ya uuzaji wa viatu tofauti.

Aprili 2020, mwezi mmoja baada ya Kenya kuthibitisha kuwa mwenyeji wa janga la Covid-19, Kimani alipoteza kazi ya uhasibu.

Mradi huo ndio ulimuajiri, na anasema hela anazotia kibindoni akilinganisha na alizokuwa akiingiza kwenye ajira, zinapiku mshahara aliokuwa akilipwa kwa kiwango kikubwa.

Huku akiridhia hatua alizopiga kimaendeleo, anasema siri kufanikisha ufugaji ni kutambua ndege au kuku wanaohitajika sokoni.

 

Peter Kimani akionyesha kuku aina ya bantams anaofuga eneo la Umoja, Nairobi. PICHA | SAMMY WAWERU

Kuku wenye umbo dogo na maridadi, aina ya silkie bantams, ni miongoni mwa wenye ushindani mkuu sokoni.

“Kando na kujua wanachohitaji wateja, fuga kwa wingi ili kutosheleza soko,” ahimiza, akishauri wafugaji chipukizi.

Kila juma, Kimani hufanya mauzo ya bantams wasiopungua 60.

Kifaranga mwenye umri wa siku moja, huuza kati ya Sh800 – 1, 000, pea ya walio miezi miwili hadi mitatu Sh6,000.

Waliokomaa, pea ya kike na kiume haipungui Sh15,000.

Aidha, yai la kuku hao halipungui Sh250.

Yote tisa, kumi Kimani anahimiza vijana wasilaze damu, wajitume katika sekta ya kilimo na ufugaji, akikiri ina mapato ya kuridhisha.

“Wasitegemee ajira za ofisi kwa sababu kwa kiasi fulani hazipatikani kwa urahisi. Wawekeze katika sekta ya kilimo-ufugaji-biashara.”

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending