Connect with us

General News

Umaskini na ukosefu wa intaneti huyumbisha elimu mtandaoni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Umaskini na ukosefu wa intaneti huyumbisha elimu mtandaoni – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Umaskini na ukosefu wa intaneti huyumbisha elimu mtandaoni

AFISA Mkuu Mtendaji wa Tume ya Huduma za Walimu (TSC), Dkt Nancy Macharia, juzi alizindua mpango ambapo walimu wataendesha mafunzo kwa njia ya dijitali katika shule za msingi na upili za umma.

Alisema kupitia mpango huo shughuli za masomo hazitasitishwa ilivyofanya wakati wa mlipuko wa janga la Covid-19 kuanzia Machi 15, 2020.

Chini ya mpango huo, Dkt Macharia alisema, walimu kutoka shule zilizo na vifaa hitaji watapeperusha vipindi vya masomo kupitia majukwaa mbalimbali ya kidijitali ili kuwafikia wanafunzi popote walipo.

Lakini Dkt Macharia asije akasahau kwamba mwaka huo wa 2020 Waziri wa Elimu George Magoha aliungama kuwa mpango sawa na huo ulifeli kutokana na umasikini na ukosefu wa intaneti haswa maeneo ya mbali na miji mikubwa.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending