Connect with us

General News

Umeme nafuu utaimarisha sekta ya viwanda na kupanua nafasi za ajira – Mbunge – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Umeme nafuu utaimarisha sekta ya viwanda na kupanua nafasi za ajira – Mbunge – Taifa Leo

Umeme nafuu utaimarisha sekta ya viwanda na kupanua nafasi za ajira – Mbunge

Na LAWRENCE ONGARO

WAMILIKI wengi wa viwanda wanangoja kushuka kwa bei ya umeme ili waweze kuongeza faida kwa bidhaa zao.

Hivi majuzi Rais Uhuru Kenyatta aliahidi Wakenya kuwa gharama na ada ya umeme itapunguzwa kwa kiwango cha hadi asilimia 30.

Serikali pia imefanya juhudi kuona ya kwamba umeme unasambazwa mashinani kwa lengo la kuboresha maendeleo.

Wamiliki wengi wa viwanda wana hamu ya kuona hatua hiyo ikitimia ili nao waweze kuongeza mapato yao kwa wingi.

Mbunge wa Thika Bw Patrick ‘ Jungle’ Wainaina, ambaye ni mfanyabiashara mashuhuri wa parachichi na macadamia, anasema iwapo hatua hiyo itatimia bila shaka viwanda vingi vitaweza kunufaika pakubwa.

“Wafanyabiashara wengi wenye viwanda wanatumia fedha nyingi kulipia umeme, na iwapo bili itashuka, kuna matumaini ya kupiga hatua zaidi,” alifafanua mbunge huyo.

Alitoa mfano ya nchi ya Afrika Kusini na Misri ambako viwanda vyao vinalipia ada ya chini ya umeme.

Alisema hata nchi ya Kenya inastahili kufuata mkondo huo ili wenye viwanda nao wapate faida zaidi.

Mbunge huyo aliyasema hayo mjini Thika alipokutana wafanyabiashara wa eneo hilo.

Alisema iwapo ada hiyo itakuwa ya chini bila shaka hata bidhaa zinazotengenezwa viwandani zitauzwa kwa bei nafuu.

Alisema nchi zilizoendelea zinakuwa na viwanda vingi kwa sababu gharama ya umeme huwa ni nafuu kwa wenye viwanda hivyo.

Alieleza nchi ya Kenya ni nchi ya viwanda vingi ambapo ada ya umeme ikishuka bila shaka viwanda vitaongezeka na vijana wengi watapata ajira.

Alieleza umeme ndio njia ya pekee itakayoboresha maisha ya wananchi kwa kujiendeleza kiajira.