– Huku bila kumjali dereva wao, jamaa na kipusa wake walianza kunyegeza kiuno wakiwa kwenye gari barabarani
– Kitendo hicho kilinaswa na kuchapishwa kwenye mtandao wa twitter ambapo moto uliwaka
– Ni kitendo ambacho kimeupa Umoja wa Mataifa jina mbaya huku madai yakiibuka kuhusu dhuluma za kimapenzi
Usherati unaendelea kuongezeka duniani kila uchao huku visa vya watu kuhusika ufuska katika maeneo yasiyofaa vikiongezejka.
Sasa wafanyakazi wawili wa shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wamejipata taabani baada ya kurekodiwa wakiwa kwenye harakati za kumumunya tunda ndani ya gari la kampuni hiyo.