[ad_1]
Unachotakiwa kufanya ili kuondoa mba kichwani
Na MARGARET MAINA
[email protected]
WATU wengi wanakabiliwa na tatizo la vipande vidogovidogo vya ngozi visivyo hai na vyenye mwonekano wa kutisha kichwani.
Kwa kiasi fulani, mba huwa ni sehemu ya asili ya ngozi yetu.
Mba husababisha mwasho kichwani.
Japo wengi wetu hudhania kwamba mba husababishwa na uchafu, ifahamike kwamba mba hasa husababishwa na ukavu wa ngozi.
Unaweza ukatumia shampoo ya kuondoa mba lakini baadhi ya aina za shampoo huwa na kemikali ambayo inaweza kukuletea matatizo ya ngozi. Ni afadhali ukatumia njia za asili.
Juisi ya limau
Unaweza ukatumia limau kuondoa mba bila kukumbwa na madhara. Asidi ya citric katika limau inasaidia kushambulia fangasi na inasaidia kupandisha ngozi zilizokufa juu na kukuwezesha kuzisafisha – kuziosha – kwa urahisi.
Kuna njia nzuri za kutumia limau. Kamua limau bila kutia chochote halafu masaji ngozi yako ya kichwa kwa kutumia maji hayo na uache kwa dakika tano.
Osha nywele zako kwa kutumia maji ambayo umechanganya na kijiko kimoja cha limau. Fanya hivi kila unapotaka kuosha nywele.
Chumvi
Chukua chumvi kisha masaji katika kichwa. Jaribu kufanya hivi kabla hujatumia njia nyingine ya kuondoa mba. Hapa ina maana kwamba unatangulia kutumia chumvi kabla ya kutumia njia nyingine ili hii njia yako ya pili iwe ya ufanisi maradufu.
Kitunguu saumu
Namna nyingine ya kuondoa mba ni kwa kutumia kitunguu saumu. Unaweza kuwaza kuhusu harufu lakini hii ni njia nzuri mno ya kuondoa mba kwa maana ina nguvu kubwa za kuondoa/kusafisha mba kwa haraka.
Twanga kitunguu saumu chako na changanya na kikombe kimoja cha maji. Masaji katika ngozi ya kichwa kisha iache kwa muda wa dakika 10.
Osha kwa kutumia shampoo.
[ad_2]
Source link