Connect with us

General News

Undumakuwili wa Ruto kuhusu hatimiliki Pwani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Undumakuwili wa Ruto kuhusu hatimiliki Pwani – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Undumakuwili wa Ruto kuhusu hatimiliki Pwani

NA CHARLES WASONGA

JUZI Naibu Rais William Ruto aliwaongoza wabunge wandani wake kutoka Pwani, kuisuta serikali kwa kushindwa kutatua changamoto ya kihistoria kuhusu umiliki wa ardhi katika eneo hilo.

Wakiongea katika uwanja wa Burhani, eneobunge la Mvita, Mombasa, walidai wakazi ni maskwota wanazongwa na umasikini baada ya serikali kufeli kuwapa hatimiliki za ardhi, ilivyoahidi hapo awali.

Lakini Dkt Ruto asije akasahau kuwa mnamo Agosti 30,2013, yeye na Rais Uhuru Kenyatta, waliongoza hafla ya utoaji hatimiliki kwa zaidi ya wakazi 60,000 wa Pwani. Shughuli hiyo iliendeshwa katika uwanja wa Karisa Maitha, Kaunti ya Kilifi.

Vile vile, takwimu kutoka Wizara ya Ardhi zinaonyesha kuwa kufikia sasa serikali ya Jubilee, ambayo Dkt Ruto anahudumia, imeendelea kutoa hatimiliki kwa wakazi wa Pwani.

Kufikia sasa serikali imetoa jumla ya hatimiliki 5, 316, 974 kote nchini, nyingi zikitolewa katika eneo la Pwani.