Connect with us

General News

Ureno wacharaza Uturuki na kuweka hai matumaini ya kuingia fainali za Kombe la Dunia – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ureno wacharaza Uturuki na kuweka hai matumaini ya kuingia fainali za Kombe la Dunia – Taifa Leo

Ureno wacharaza Uturuki na kuweka hai matumaini ya kuingia fainali za Kombe la Dunia

Na MASHIRIKA

URENO waliweka hai matumaini ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mnamo 2022 baada ya kukomoa Uturuki 3-1 mnamo Alhamisi usiku katika nusu-fainali ya mchujo jijini Porto.

Mabao ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Otavio Edmilson na Diogo Jota yaliwaweka wenyeji Ureno kifua mbele katika kipindi cha kwanza ugani Do Dragao.

Ingawa Uturuki walirejea mchezoni kupitia kwa Burak Yilmaz kunako dakika ya 65, Matheus Nunes alizamisha kabisa chombo cha wageni wao mwishoni mwa kipindi cha pili.

Chini ya kocha Fernando Santos, Ureno kwa sasa watavaana na Macedonia Kaskazini katika fainali ya mchujo ili kuwania tiketi ya kuelekea Qatar kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia kati ya Novemba na Disemba 2022.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending