Connect with us

General News

Usajili wa boda kusaidia vita dhidi ya ugaidi – Serikali – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Usajili wa boda kusaidia vita dhidi ya ugaidi – Serikali – Taifa Leo

Usajili wa boda kusaidia vita dhidi ya ugaidi – Serikali

NA KALUME KAZUNGU

IDARA ya usalama katika Kaunti ya Lamu inatarajiwa kuwa usajili wa wahudumu wa bodaboda utasaidia kupigana na kero la ugaidi eneo hilo.

Jumatatu, serikali ya kitaifa ilianzisha usajili wa wahudumu wa bodaboda kote nchini kama njia ya kulainisha sekta hiyo inayotajwa kuwa na doa.

Akizungumza wakati alipoongoza uzinduzi wa shughuli hiyo kwenye kituo cha Huduma Centre kilicho kisiwani Lamu, Kamishna wa Kaunti ya Lamu, Bw Irungu Macharia alisema mpango huo utasaidia pia kiusalama.

Kulingana naye, magaidi wa Al- Shabaab ambao hushukiwa kujifi – cha ndani ya sekta hiyo sasa hawatapata nafasi.

Kamishna huyo alisema wanalenga kusajili angalau bodaboda 2,000 kufikia mwisho wa kipindi cha siku 60 zilizotengwa.

Bw Macharia alisisitiza kuwa siku hizo zilizotengwa na serikali zitakapoisha, wale ambao hawatakuwa wamejisajili hawataweza kufanya biashara ya uchukuzi wa bodaboda.

“Nimefurahia mpango huu wa serikali. Mahali kama hapa Lamu tunaamini utasaidia pakubwa kufaulisha vita dhidi ya ugaidi. Utatuwezesha kufuatilia moja kwa moja na kunasa washukiwa wanaojifi – cha ndani ya sekta hii,” akasema Bw Macharia.

Serikali hiyo pia imeahidi kuhakikisha bodaboda 200,000 watakaosajiliwa kwanza kwenye shughuli hiyo wanafadhiliwa kwenye mpango wa Bima ya Kitaifa ya Afya (NHIF) kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Bw Macharia aliwahimiza wahudumu kuchukua nafasi za kwan katika kusajiliwa ili wanufaike na ufadhili wa serikali wa bima hiyo ya bure ya NHIF.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa wahudumu wa bodaboda kisiwani Lamu, Bw Abdallah Bakari, alipongeza shughuli hiyo ya usajili, akisema tayari amekuwa akiendeleza kampeni kwa wanachama wake kuukumbatia mpango huo.

Bw Bakari hata hivyo aliisihi idara ya usalama na maafisa husi – ka wa mpango huo kuhakikisha ni bodaboda halali pekee ndio wanaosajiliwa.

“Ikiwa kila mtu atajitokeza kusajiliwa kiholela kama bodaboda kwenye mpango huu, ikiwemo wahalifu, huenda lengo la mpango huu lisiafikiwe,” akasema Bw Bakari.

Shughuli hii inajiri baada ya kisa ambapo mwanamke alivamiwa jijini Nairobi baada ya kuhusika kwenye ajali ndogo na mwendeshaji bodaboda.

Tukio hilo lilisababisha lalama tele kitaifa kuhusu jinsi sekta hiyo inavyozidi kupanuka bila mfumo bora wa kuudhibiti ipasavyo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending