Connect with us

General News

Usajili wa mitihani ya kitaifa 2022 kuanza Jumatano – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Usajili wa mitihani ya kitaifa 2022 kuanza Jumatano – Taifa Leo

Usajili wa mitihani ya kitaifa 2022 kuanza Jumatano

NA WINNIE ONYANDO

USAJILI wa watahiniwa kwa Mitihani ya Kitaifa ya 2022 ya gredi ya sita, KCPE na KCSE utaanza Jumatano ijayo Aprili 27, 2022, Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (KNEC), Dkt David Njengere ametangaza.

Akizungumza Jumamosi wakati wa kutolewa rasmi kwa matokeo ya mtihani wa kitaifa wa KCSE 2021 jijini Nairobi, Dkt Njengere alisema kuwa, usajili huo utakamilika mnamo Mei 14, 2022.

Kadhalika, alitoa wito kwa wazazi na walimu kuhakikisha kuwa watahiniwa wamesajiliwa kabla ya tarehe hiyo.

“Kila Mwalimu Mkuu wa shule ahakikishe kuwa watahiniwa wote wa Gredi ya Sita, Darasa la Nane na Kidato cha Nne wamesajiliwa kabla ya shughuli hiyo kufungwa.

Kadhalika, wazazi pia wahakikishe kuwa watoto wao wamesajiliwa,” akasema Dkt Njengere.

“Hatutaki kushuhudia sarakasi za dakika za mwisho. Wadau husika wafanye mipango yao na wahakikishe kuwa wanafanya usajili ndani ya muda huo uliotengwa.”

Alisema kuwa, baraza hilo halitaruhusu usajili wa kuchelewa, na kutoa wito kwa wazazi na walezi washirikiane kwa karibu na wakuu wa taasisi ili kuhakikisha kwamba, wanafunzi wote wamesajiliwa ipasavyo.

Akisisitiza umuhimu wa usajili, huo, Katibu wa Elimu ya Msingi, Dkt Julius Jwan alisema kuwa shughuli hiyo ni ya bila malipo na akawataka wazazi kutohadaiwa na kulazimishwa kulipa ada yoyote.

“Shughuli ya usajili hailipiwi. Mtu asikubali kuahadaiwa,” akasema Dkt Njengere. Kadhalika, alisema kuwa shughuli hiyo itafanyika katika ofisi zilizotengwa kwa shughuli hiyo na KNEC.

Dkt Juan alisema serikali imejitolea kuhakikisha watoto wote watafanya mitihani ya kitaifa akisema imetenga pesa za kufadhili mitihani ya kitaifa kwa shule zote za umma na za kibinafsi.

Alisema kwamba, serikali imekuwa ikigharimia mitihani kwa zaidi ya miaka sita sasa na hakuna mzazi anayepaswa kutozwa chochote. Idadi ya watahiniwa waliofuzu kujiunga na vyuo vikuu vya umma nchini ilipungua ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending