Connect with us

General News

Usalama wa raia utiliwe maanani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Usalama wa raia utiliwe maanani – Taifa Leo

TAHARIRI: Usalama wa raia utiliwe maanani

NA MHARIRI

SERIKALI inahitajika ikaze kamba kuhusu kukabiliana na visa vingi vya uhalifu ambavyo vinaendelea kutokea nchini.

Katika miezi ya hivi majuzi, ripoti kuhusu uhalifu hasa mauaji zimezidi kwa kiwango cha kutisha.

Wananchi wengi wamepoteza maisha yao na mali zao kuharibika wanapovamiwa na makundi ya wahalifu katika pembe tofauti za nchi, huku wengine wakipatikana wameuawa baada ya kutoweka ghafla.

Katika baadhi ya maeneo nchini, mashambulio yamekuwa yakitendwa na makundi ya kigaidi huku katika maeneo mengine, yalifanywa na makundi ya wahalifu ambao wakati mwingi huwa wamechochewa dhidi ya jamii nyingine na pia kuna mauaji ambayo chanzo chao hakieleweki.

Haya ni maovu ambayo yamekuwa yakijirudia sana tangu miaka iliyopita na ingetarajiwa yawe yamepungua kwa kiwango kikubwa au hata kukomeshwa kabisa kufikia sasa.

Hairidhishi kila mara tunaposikia serikali inavyotaja miji mikuu kama mifano ya maeneo ambapo mashambulio aina hiyo yamezuiwa.

Hatukatai kwamba maafisa serikalini wana haki ya kusifu mikakati walioeka, kwa mfano katika kuzuia mashambulio ya kigaidi katika miji mikubwa ya nchi, lakini inafaa tukumbuke kwamba pia wale wananchi ambao wanaishi maeneo ya mbali wana kila haki ya kulindwa kikamilifu.

Mojawapo ya mbinu ambazo zinafaa kutiliwa maanani katika juhudi za kuimarisha usalama, ni uwekezaji katika ukusanyaji wa habari za kijasusi.

Idara ya usalama ni mojawapo ya zile ambazo hupewa bajeti kubwa ya taifa na hivyo basi raia wanahitaji kuona kwamba fedha hizo zinazotoka kwa ushuru wanaotozwa zinatumiwa vyema.

Katika miaka iliyopita, chini ya utawala wa Rais Uhuru Kenyatta, taifa hili liliona mabadiliko mengi yakitekelezwa katika idara ya usalama kwa lengo la kuboresha utoaji usalama kwa umma.

Inatarajiwa kuwa mojawapo ya sehemu ambazo ziliboreshwa ni idara zote za kukusanya habari za kijasusi, iwe ni kuhusu matukio ya ndani ya nchi au yale ya mpakani ili kuzuia ghasia na mashambulio.

Hivyo basi, uwekezaji huu unafaa kuonyesha matokeo bora sio tu kwa utulivu wa miji mikuu bali katika pembe zote za nchi, kwani ni rahisi ukosefu wa usalama unaoshuhudiwa mbali uenee hadi maeneo mengine ikiwa hatutakuwa waangalifu.

Tunapoelekea katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti, suala la usalama ni mojawapo ya yale yanayofaa kuchukuliwa kwa uzito kutokana na kuwa wahalifu hutaka kutumia kipindi hiki kutekeleza maovu yao.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending