Connect with us

General News

Ushuru wa VAT, PAYE usitishwe – Wanaharakati – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ushuru wa VAT, PAYE usitishwe – Wanaharakati – Taifa Leo

Ushuru wa VAT, PAYE usitishwe – Wanaharakati

NA WACHIRA MWANGI

WANAHARAKATI wa kutetea haki za kibinadamu katika eneo la Pwani wameitaka serikali kusitisha kwa muda ushuru wa bidhaa muhimu na ule unaotozwa kutoka kwenye mishahara (PAYE) ili kuwakinga raia dhidi ya gharama ya juu ya maisha.

Wanaharakati hao walikongamana katika barabara ya Moi Avenue jijini Mombasa huku wakiwa wamevalia magunia na kubeba sahani na masufuria matupu wakiimba: ‘Punda amechoka’ na ‘Bila chakula hakuna kura’.

Wakiongozwa na Bw Hussein Khalid wa shirika la HAKI Africa na vuguvugu la Kutetea Haki Pwani (PSJCWG) linalojumuisha mashirika 17, wanaharakati hao walilalamikia ongezeko la bei ya bidhaa muhimu.

“Maisha yamekuwa magumu na hali inazidi kuzorota. Wakenya wanalia kila mahali kwa sababu hawana chakula. Lakini viongozi wako kimya,” akasema Bw Khalid.

Alisema kusitishwa kwa ushuru huo kutawezesha bei ya bidhaa muhimu kushuka.

“Maisha yanazidi kuwa magumu kila uchao. Gharama ya bidhaa inaongezeka kila siku na wazazi wameshindwa kulisha familia zao,” akasema Bw Khalid.

Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa zaidi ya Wakenya milioni 3.5 wanahitaji chakula kwa dharura kufuatia ukame ambao unaendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Kaunti 23 hasa katika maeneo kame ndizo zimeathiriwa zaidi na makali ya njaa.

Bei ya bidhaa muhimu kama vile mafuta ya kupikia, gesi, mkate, maziwa, sukari imeongezeka kwa kiasi kikubwa ndani ya miezi miwili iliyopita.

Kwa mfano, pakiti moja ya maziwa ya mililita 400 sasa inauzwa kwa Sh60 badala ya Sh50 mwezi uliopita wa Machi.

Mtungi wa gesi ya kilo 13 sasa unauzwa kwa Sh3,200 badala ya Sh1,800 miezi mitatu iliyopita.

Mswada wa Fedha uliowasilishwa Bungeni na waziri wa Fedha, Ukur Yatani unapendekeza kuongezwa kwa ushuru wa Thamani ya Ziada (VAT) kwa asilimia 10 kuwezesha serikali kupata mapato ya Sh50.4 bilioni zaidi.

Bidhaa zinazolengwa katika mswada huo ni bia, sigara, juisi ya matunda na maji ya chupa.

Wanaharakati hao walisema kuwa baa la njaa limewasababishia mamilioni ya Wakenya mateso tele na limechangia katika ongezeko la visa vya utovu wa usalama katika maeneo kame.

“Kifungu cha 43 cha Katiba kinataka kila Mkenya kupata chakula bora na cha kutosha. Hivyo serikali haina budi kusitisha kwa muda ushuru wa VAT kwa bidhaa muhimu na PAYE ili wananchi wapate hela za kukabiliana na hali ngumu ya maisha,” akasema.

Wanaharakati hao waliapa kuendelea kuandamana kila wiki hadi pale serikali itakaposhughulikia malalamishi yao kwa kupunguza gharama ya maisha na kuwezesha kila Mkenya kupata chakula cha kutosha.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending