Uvumilivu ulivyompa Marionex fursa ya kufanya kazi na wasanii maarufu nchini
Na JOHN KIMWERE
HILDAH Nasimiyu Wanjoya maarufu Marionex ni kati ya wasanii wa kike wanaoibukia kama video vixen nchini Kenya.
Licha ya virusi vya corona kuvuruga shughuli za burudani anaamini hali itakuwa sawa.
Ingawa ndoto yake ya tangu utotoni ilikuwa kuhitimu na kuwa mwanahabari, anasema amejifunza mengi kuhusu taaluma yake.
”Bila kuiga matamshi ya naibu rais, William Ruto ukweli wa mambo kazi ni kazi bora iwe inakuletea mkate mezani,” anasema na kuongeza kuwa binafsi hufurahia kuwa kati ya warembo wa kunogesha nyimbo za wasanii wa kizazi kipya.
Mejja
Aidha anasema kuwa mradi sio shughuli haramu kwake ni ajira. Alianza kujituma kwenye masuala ya video vixen mwaka 2018 japo alikuwa akishiriki nyimbo za wasanii wanaokuja.
Ndani ya muda huo tayari amefanikiwa kushiriki nyimbo za kati ya wasanii wanaopiga hatua katika jukwaa la muziki wa burudani nchini.
Ameshiriki nyimbo kama: Lewa- Mejja ft Wanati, Kwa kwa kwa-Vdj Jones ft Wakali, This Love-Wahu, Why lie-Alphajiri ft Kidum, Joni-Mejja ft Wanati, Waka waka-Jegede ft Elehai Kabagazi, Dj Gogez.
Ingawa ndio ameanza kupiga ngoma ambapo hajaona matunda ya taaluma yake anasema kwa kumtazamo wake inalipa anakomwomba Maulana amjalie ndani ya siku zijazo.
Hildah Nasimiyu Wanjoya maarufu Marionex video vixen anayekuja. PICHA | JOHN KIMWERE
Katika mpango mzima dada huyu anasema anashiriki taaluma ya video vixen akilenga kutinga upeo wa kati ya wasanii mahiri duniani Selena Gomez mzawa wa Marekani.
Je ili kuwa video vixen mzuri ni vigezo gani mshiriki anapaswa kuwa navyo?
Binti huyu mwenye tabasamu ya kuvutia anasema baadhi yavyo ni muonekano mzuri, mavazi bila kuweka katika kaburi la sahau ubunifu.
Urembo wa mabinti wengi huchangia wanaume kuchemka damu muda tu wanapowaona hali ambayo hufanya baadhi yao kujikuta wakifanya michepuko.
Dada huyu anasema anapenda sana kuheshimiwa maana naye pia anaheshimu mwili wake kuliko maji yake. Hata hivyo hawezi kusahau kuna wakati alilia kwa sababu ya mapenzi alipogundua kuwa mpenzi wake hakuwa anampenda alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana mwingine.
Anashauri wenzake wawe wavumilivu pia wajitume na kujiamini wanaweza kwa chochote wanachofanya pia ipo siku watatimiza azma yao.
Sina budi kutaja kuwa serikali inapaswa kuwa mstari wa kwanza kusapoti sekta ya burudani kwa kuzingatia imekaa vizuri kutoa ajira kwa wasanii wengi tu wanaume na wanawake.
Changamoto
“Wasanii chipukizi tunapitia wakati mgumu kwa kuzingatia tunahitaji kujibrandi ilhali hatuna ajira ya kulipa mshahara mzuri kugharimia mahitaji yote. Huwa tunahitaji mavazi mazuri, kuchukua picha za mitindo tofauti kwa ajili ya kuzisambaza mitandaoni kutangaza kazi yetu,” anasema na kuongeza kwamba wapo wengine huwaonyesha dharau.