Connect with us

General News

Uzalishaji wa mahindi, maharagwe na ngano washuka, bei zaongezeka – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Uzalishaji wa mahindi, maharagwe na ngano washuka, bei zaongezeka – Taifa Leo

Uzalishaji wa mahindi, maharagwe na ngano washuka, bei zaongezeka

NA BRIAN AMBANI

BEI ya vyakula nchini imepanda kutokana na kuongezeka kwa gharama ya uzalishaji kwa asilimia 11.3 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Takwimu za Taasisi ya Kitaifa ya Data (KNBS) zinaonyesha kuwa bei ya uzalishaji wa chakula nchini (PPI) ambayo huathiri gharama ya bidhaa moja kwa moja, ilipanda kwa asilimia 5.67 kati ya Desemba 2021 na Machi 2022.

Haya yanajiri huku wafanyibiashara wakikabiliwa na kupanda kwa gharama ya bidhaa za kimsingi zinazoagizwa kutoka nje ya nchi kama vile mahindi na ngano kutokana na uhaba katika soko la kimataifa kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

Mwaka 2021, Kenya ilitegemea bidhaa za kuagizwa nje ya nchi huku kilimo cha ndani kikitatizwa na uhaba wa mvua.

Utafiti wa uchumi unaonyesha uzalishaji wa mahindi ulipungua kwa asilimia 12.8 kutoka magunia milioni 42.1 mnamo 2020 hadi magunia milioni 36.7 mwaka 2021.

Kadhalika, uzalishaji wa maharagwe na ngano ulishuka kwa asilimia 14 na asilimia 39.4 mtawalia. Hii imefanya gharama ya bidhaa kama vile unga, mkate na maziwa kupanda.

 

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending