[ad_1]
Video ya ‘njama’ ya shahidi dhidi ya Ruto ICC kuchezwa
NA JOSEPH WANGUI
MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imekubali ombi la wakili Mkenya, Paul Gicheru ili kanda ya video inayoonyesha jinsi mashahidi walivyokuwa wakiandaliwa na wachunguzi kabla ya kuandikisha taarifa itumike kortini kufifisha kesi yake.
Jaji Miatta Maria Samba aliamrisha upande wa mashtaka uruhusu video hiyo ichezeshwe kortini huku kesi inayomkabili Bw Gicheru ikianza kusikilizwa hapo Jumanne ijayo, jijini Hague, Uholanzi.
Shahidi ambaye yuko kwenye video hiyo alikuwa ametoa ushahidi katika kesi ya Naibu Rais, Dkt William Ruto na Mwanahabari Joshua Sang’ miaka saba iliyopita ambaye baadaye korti iliamua kuwa hakuwa shahidi wa kutegemewa.
Stakabadhi zilizopo mahakamani zinaonyesha kuwa shahidi huyo alikuwa ametoa ushahidi ambao hauthibitiki ilhali alikuwa amekula kiapo huku ikibainika baadaye kuwa ushahidi wake ulitoka kwa mtu ambaye hakutambuliwa kortini.
Jaji Miatta aliamuru upande wa mashtaka uchukue sehemu ya video hiyo ambayo itawafaa kisha kufichua kwa upande wa utetezi kabla ya Februari 14, 2022.
“Korti haikubaliani na Kiongozi wa Mashtaka kuwa tayari upande wa utetezi una video hiyo. Hata hivyo, hauna iliyotumika katika kesi ya Ruto na Sang,” akasema Jaji huyo akisisitiza kuwa upande wa utetezi lazima uwasilishe ushahidi katika kesi hiyo na video hiyo huenda ikasaidia katika kufahamu ukweli katika kesi hiyo.
Kesi ya Bw Gicheru itaanza kusikizwa Februari 15 ila upande wa mashtaka unaonekana kutatizika katika kujenga kesi thabiti dhidi yake baada ya mashahidi kadhaa kujiondoa.
Upande wa mashtaka unaongozwa na James Steward ambaye ni naibu kiongozi wa mashtaka.
Mwanzoni ilikadiriwa kuwa mashahidi 13 wangeitwa kutoa ushahidi katika kesi hiyo ila wengi wao wanaonekana kughairi nia na kukoma kushirikiana na korti.
Next article
Omamo ajitetea kuhusu kesi ya Miguna kurejea Kenya
[ad_2]
Source link