Connect with us

General News

Viongozi wa kidini wakosoa wanasiasa kuhusu kampeni za mapema za uchaguzi mkuu 2022 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Viongozi wa kidini wakosoa wanasiasa kuhusu kampeni za mapema za uchaguzi mkuu 2022 – Taifa Leo

Viongozi wa kidini wakosoa wanasiasa kuhusu kampeni za mapema za uchaguzi mkuu 2022

BRIAN OJAMAA na MARY WANGARI

MUUNGANO WA MAKANISA na Viongozi wa Kidini Nchini (CCAK) umehimiza viongozi kujiepusha na kampeni za mapema zinazoweza kusababisha michafuko nchini huku ukikashifu kisa ambapo mkutano wa Naibu Rais William Ruto ulivurugwa Kisumu.

Kwenye taarifa jana, CCAK ilitoa wito kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Tume ya Ushikamano na Maridhiano (NCIC) Idara ya Polisi na mashirika mengineyo, kushirikiana kuwaadhibu wanaosababisha migawanyiko na utengano.

“CCAK inalaani ghasia za kisiasa zilizoshuhudiwa Kisumu ambapo mkutano wa Naibu Rais ulikatizwa na kundi lililokuwa likirusha mawe. Sote tunataka kuona taifa ambapo kampeni zinaendeshwa bila ghasia hata wakati watu wanatofautiana kisera na kimtazamo,”ilisema CCAK.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglican Kenya, Jackson Olesapit, alisema Uchaguzi Mkuu ujao ungali mbali na wanasiasa wanapaswa kufuata kalenda ya (IEBC) kuhusu kampeni.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending