Connect with us

General News

Viongozi wanaofaa wataipa sura mpya AFC Leopards – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Viongozi wanaofaa wataipa sura mpya AFC Leopards – Taifa Leo

Viongozi wanaofaa wataipa sura mpya AFC Leopards

NA JOHN ASHIHUNDU

SIKU zinakaribia kwa mashabiki wa klabu ya AFC Leopards kuchagua viongozi watakaoongoza klabu hiyo kwa miaka mitatu.

Leopards inatarajia kufanya uchaguzi huo mnamo Juni 23, lakini mwezi huu wa Aprili ndio wa mwisho kwa wapiga kura kujiandikisha ili wakubaliwe kushiriki kwenye zoezi hilo linalotarajiwa kuvutia mabwanyenye kadhaa, akiwemo Maurice Amahwa.

Ni vyema iwapo mashabiki watajiandikisha kwa wingi ili wapate fursa ya kuchagua viongozi kuanzia mashinani ambao watajitolea kuibadilisha timu hii kongwe na kuipatia sura mpya.

Kwa miaka mingi, Leopards na Gor Mahia zimekuwa na umaarufu mkubwa wa kimataifa, lakini zimekuwa zikififia kutokana na hali ngumu ya kiuchumi.

Leopards imekuwa ikumbayumba kutokana na ukosefu wa fedha za kugharamia mahitaji ya wachezaji pamoja na uongozi duni, hasa miaka ya karibuni kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kuzuka kwa ugonjwa wa Covid-19.

Tunatarajia ushindano mkali, lakini ni jukumu la mashabiki kufanya uchaguzi kwa makini ili wapate watu sahihi ambao wataleta klabu hiii mabadiliko yanayofaa.

Viongozi sahihi wataiwezesha Ingwe kupata wadhamini wa kusaidia timu hii kongwe iliirejeshe makali yake yanayozidi kudidimia kila wakati.

Katika miaka ya karibuni, Leopards imekuwa ikipata watu wenye tamaa ya kujinufaisha ambao haja yao imekuwa kujijengea majina klabuni na baadaye kuwania vyeo vya kisiasa.

Zaidi ya mashabiki milioni sita wa Ingwe kutoka pembe zote wanapaswa kujiandikisha kwa wingi ili kuwezesha timu yao kukabiliana vyema na matatizo ya kifedha.

Kwa miaka ya karibuni, uchaguzi wa Leopards umekuwa ukishirikisha wanachama wasiozidi 1,000 ambao ni rahisi kununuliwa na watu wenye tamaa ya uongozi ambao baadaye wanashindwa kutekeleza wajibu wao.

Itakuwa vyema iwapo wasimamizi wa uchaguzi huo watafanya juhudi kuhakikisha ni wanachama halisi pekee wanaokubaliwa kushiriki katika uchaguzi ujao.

Ni vyema iwapo orodha ya wanachama itatolewa mapema, na ikiwezekana ada ya kushiriki kwenye uchaguzi huo ingepunguzwa kutokana na hali ngumu ya maisha inayokabiliwa mashabiki kwa jumla.

Afisi ya sasa ya Dan Shikanda iliwekwa mamlakani kwa njia ya kutatanika mnamo 2019, hali ambayo ilichangia mvutano kati ya afisi hiyo na Afisi ya Msajili wa Vyama vya Starehe baada ya kundi Fulani ya washikaji dau kupinga kuchaguliwa kwao.

Kulingana na Sheria Mpya ya Michezo, ili klabu kama Leopards iandae uchaguzi wa hali ya ukweli, ni lazima orodha iwe na wanachama kutoka angalau kaunti 24 za nchi.

Lakini takwa hilo lilipuuzwa na waliosimamia uchaguzi huo wa kutatanisha, na klabu ilikaribiwa kujitumbukiza mashakani kisheria.

Mwanzo, washikaji dau hao walikuwa wamepinga kwamba kamati iliyoteuliwa kusimamia uchaguzi huo ilikuwa ikipendelea upande mmoja, lakini wanachama Fulani walikimbia uwanjani na kuchagua kundi la Shikanda kwa haraka na kumaliza shughuli hiyo.

Wafuasi hao wa Ingwe waliwasilisha malalamishi yao baada ya kugundua kwamba majina ya wanachama kadhaa yalikuwa yameondolewa orodhani.

Serikali ilikuwa imeiagiza klabu iwasilishe majina ya wanchama walio hai ili washiriki kwenye uchaguzi huo.

Chini ya sheria mpya ambayo kwa sasa inapingwa vikali na wanachama, ni maafisa watatu tu waliochaguliwa Shikanda kama mwenyekiti, Oliver Sikuku (Katibu Mkuu) na Maurice Chichi (Mweka Hazina).

Kupitia kwa afisi ya Msajili wa Vyama Rose Wasike, uchaguzi huo haukufanyika kisheria na ikaupiga marufuku, lakini Shikanda na kundi lake alikataa kufuata sheria, wakati Wasike aliitaka kamati ya Dan Mule ibakie usukani hadi uchaguzi halali ufanyike.

Jinsi mambo yalivyo kwa sasa, kamati ya Shikanda imeshindwa kuongoza vyema, kiasi cha kusababisha migomo ya mara kwa mara ya wachezaji ambao wanadai marupurupu yao ya miezi kadhaa.

Ni jambo la kushangaza kwamba baadhi ya wachezaji wanadai klabu marupurupu yao ya tangu 2020!

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending