Connect with us

General News

Vipusa wa Chelsea waponda Leicester na kutua kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Vipusa wa Chelsea waponda Leicester na kutua kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu

Vipusa wa Chelsea waponda Leicester na kutua kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu

Na MASHIRIKA

WAREMBO wa Chelsea walitua kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (WSL) kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kuponda Leicester City 9-0 uwanjani King Power mnamo Jumapili usiku.

Chelsea waliweka rekodi ya kuwa kikosi cha kwanza kuwahi kufunga mabao matatu chini ya dakika 10 za mchuano wa WSL. Magoli hayo yalipachikwa wavuni kupitia Guro Reiten, Sam Kerr na Beth England. Aniek Nouwen alicheka na nyavu kabla ya England, Reiten na Kerr kukamilisha mchuano huo na magoli mawili kila mmoja. Lauren James na Jessie Fleming walitokea benchi na kufunga bao kila mmoja.

Chelsea waliwaruka Arsenal kileleni mwa jedwali baada ya mchuano kati ya wanabunduki hao na Tottenham Hotspur kuahirishwa kutokana na wingi wa visa vya maambukizi ya virusi vya corona kambini mwa Spurs. Ushindi wa Chelsea uliendeleza ubabe wao dhidi ya Leicester ambao pia walipokezwa kichapo cha 7-0 kutoka kwa Chelsea kwenye raundi ya tano ya Kombe la FA mnamo Februari 2022.

Chini ya kocha Emma Hayes, Chelsea kwa sasa hawajapoteza mechi yoyote kati ya nane zilizopita ligini. Wameshinda michuano mitano iliyopita katika mashindano yote na wanajivunia pengo la alama moja kati yao na Arsenal kileleni mwa jedwali. Zimesalia mechi tano pekee kabla ya kampeni za WSL msimu huu kutamatika rasmi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending