-Wagonjwa 49 walipona virusi hivyo na kuruhusiwa kuenda nyumbani, idadi ya waliopona ikifikia 2,881
– Mgonjwa mmoja aliaga dunia, idadi jumla ya vifo kutokana na virusi hivyo ikifikia 185
– Nairobi inaongoza na visa 209 ikifuatwa na Kiambu (49) na Busia (38)
Idadi ya visa vya virusi vya corona nchini imefika 10,000 baada ya watu wengine 379 kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo na kupelekea idadi jumla kutimu 10,105.
Visa hivyo 379, viligunduliwa baada ya Wizara ya Afya kufanyia vipimo sampuli 7,050 huku idadi ya sampuli zilizokaguliwa tangu kuzuka kwa virusi hivyo ikifikia 215,037.
Wakati huo huo, habari njema ni kwamba wagonjwa 49 walipona virusi hivyo na kuruhusiwa kuenda nyumbani na idadi ya waliopona kufikia 2,881, huku mgonjwa mmoja akiaga dunia na idadi ya vifo kufika 185.
Visa hivyo katika kaunti ni kama ifuatavyo; Nairobi inaongoza na visa 209, Kiambu (49), Busia (38), Migori (19), Mombasa (16), Kajiado (12), Uasin Gishu (8), Lamu (6), Machakos na Nakuru visa vitano kila mmoja, Narok, Wajir na Kisumu visa viwili kila mmoja na Garissa, Isiolo, Kericho, Nyamira, Nyeri na Trans Nzoia zikirekodi kisa kimoja kila mmoja.
Katika kaunti ya Nairobi, eneo bungel la Kibra ndilo linaongoza na visa 52 vya maabukizi, huku Kiambu, eneo la Ruiru ndio linaongoza na visa 16.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.